Waziri wa Fedha, Mhe. Khamis Mussa Omar (Mb) (Kulia), akipokea Zawadi ya picha kutoka kwa Katibu Mkuu wa Shirika la Forodha Duniani (World Customs Organization-WCO), Bw. Ian Saunders, wakati wa Mkutano wa 32 wa Baraza la Uongozi la Shirika la Forodha Duniani Kanda ya Mashariki na Kusini mwa Afrika (WCO ESA) unaofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Hoteli ya Golden Tulip iliyopo karibu na Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume-Zanzibar.

Waziri wa Fedha, Mhe. Khamis Mussa Omar (Mb) (Katikati), akipokea tuzo ya kutambua mchango wake katika masuala ya Forodha kutoka kwa Kamishna wa Mamlaka ya Mapato ya Afrika Kusini, Dkt. Nqobani Makhubu (Kulia), wakati wa Mkutano wa 32 wa Baraza la Uongozi la Shirika la Forodha Duniani Kanda ya Mashariki na Kusini mwa Afrika (WCO ESA) unaofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Hoteli ya Golden Tulip iliyopo karibu na Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume-Zanzibar. Kushoto ni Kamishna wa Forodha na Ushuru wa Bidhaa wa Mamlaka ya Mapato Tanzania -TRA, Bw. Juma Bakari.

Waziri wa Fedha, Mhe. Khamis Mussa Omar (Mb), akizungumza jambo wakati akihutubia katika Mkutano wa 32 wa Baraza la Uongozi la Shirika la Forodha Duniani Kanda ya Mashariki na Kusini mwa Afrika (WCO ESA) unaofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Hoteli ya Golden Tulip iliyopo karibu na Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume-Zanzibar, ambapo amelishauri Baraza la Uongozi la Shirika hilo, kuja na mwarobaini wa kukabiliana na changamoto zinazokwaza ufanisi wa ufanyaji biashara ya kimataifa miongoni mwa nchi wanachama wa Baraza hilo.

Kamishna wa Mamlaka ya Mapato Tanzania-TRA, Bw. Yusuph Juma Mwenda, akizungumza wakati wa Mkutano wa 32 wa Baraza la Uongozi la Shirika la Forodha Duniani Kanda ya Mashariki na Kusini mwa Afrika (WCO ESA) unaofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Hoteli ya Golden Tulip iliyopo karibu na Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume-Zanzibar, ambapo amelishauri Baraza la Uongozi la Shirika hilo, kuja na mwarobaini wa kukabiliana na changamoto zinazokwaza ufanisi wa ufanyaji biashara ya kimataifa miongoni mwa nchi wanachama wa Baraza hilo.

Katibu Mkuu wa Shirika la Forodha Duniani (World Customs Organization-WCO), Bw. Ian Saunders, akizungumza jambo wakati wa Mkutano wa 32 wa Baraza la Uongozi la Shirika la Forodha Duniani Kanda ya Mashariki na Kusini mwa Afrika (WCO ESA) unaofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Hoteli ya Golden Tulip iliyopo karibu na Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume-Zanzibar.
Waziri wa Fedha, Mhe. Khamis Mussa Omar (Mb) (Katikati aliyeketi) akiongoza Meza Kuu katika picha ya pamoja na wataalamu wa Forodha kutoka nchi wanachama wa Shirika la Forodha Duniani Kanda ya Mashariki na Kusini mwa Afrika (WCO ESA), wakati wa Mkutano wa 32 wa Baraza la Uongozi la Shirika hilo, unaofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Hoteli ya Golden Tulip iliyopo karibu na Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume-Zanzibar.
(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, WF, Zanzibar)