WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba, ameshiriki ibada ya Jumapili, leo, Aprili 26, 2026, katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dayosisi ya Mashariki na Pwani (DMP), Usharika wa Azania Front, jijini Dar es Salaam.
Ibada hiyo iliongozwa na Katibu wa Umoja wa Utume wa Injili (United Evangelical Mission – UEM) Kanda ya Afrika, Dkt. Ernest Kadiva, kwa kushirikiana na Mchungaji Kiongozi wa KKKT Usharika wa Azania Front, Victor Makundi.




.jpeg)
