Featured Kitaifa

OFISI YA RAIS,UTUMISHI YAOMBA TRILIONI 1.5 KWA MWAKA 2026/27

Written by Alex Sonna

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Ridhiwani Kikwete, akiwasilisha Hotuba ya Bajeti kwa Mwaka wa Fedha 2026/2027 leo Aprili 17,2026 bungeni Dodoma.

Na.Alex Sonna,Mzalendo blog-DODOMA

OFISI   ya Rais, Ikulu na Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora imeliomba Bunge kuidhinisha jumla ya shilingi trilioni 1.5 kwa ajili ya matumizi ya ofisi hiyo katika mwaka wa fedha 2026/2027, ikiwa ni sehemu ya kuimarisha utekelezaji wa majukumu ya kiutawala na utoaji wa huduma kwa wananchi.

Hayo yamesemwa leo Aprili 17, 2026 bungeni Dodoma na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Ridhiwani Kikwete, wakati akiwasilisha hotuba ya bajeti ya wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2026/2027.

Amesema kati ya fedha hizo, shilingi trilioni 1.4 zimetengwa kwa ajili ya matumizi ya kawaida, huku shilingi bilioni 163 zikiwekwa kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo.

About the author

Alex Sonna