Featured Kitaifa

DKT. MIGIRO AFIKISHA SALAMU ZA RAIS DKT. SAMIA KWA MABALOZI DODOMA

Written by Alex Sonna

 

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM),Balozi Dkt. Asha-Rose Migiro, amezungumza na Mabalozi wa Mashina wa mkoa wa Dodoma wakati akiendelea na ziara yake ya kukiunganisha chama na Mashina.

Dkt. Migiro amewasilisha salamu hizo za shukrani kutoka kwa Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan, akiwashukuru Mabalozi kwa kazi kubwa wanayoifanya ya kukijenga Chama.

Akizungumza na Mabalozi wa mashina mkoani Dodoma leo Januari 20,2026 , Dkt. Migiro pia ametumia fursa hiyo ya kuwapongeza na kuhawahimiza kufanya kazi kwa kujitoa, maana uimara wa chama unaanzia ngazi ya chini kwenda juu.

About the author

Alex Sonna