Featured Kitaifa

UTUMISHI KUZINGATIA AFYA NA USALAMA WA WATUMISHI MAHALA PA KAZI

Written by mzalendo

Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw. Xavier Daudi akisisitiza jambo wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo na kuimarisha utendaji kazi kwa watumishi wa ofisi hiyo yaliyofanyika katika Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma.

Sehemu ya Wakurugenzi na watumishi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, wakifuatilia mafunzo kuhusu usalama na afya mahali pa kazi yaliyofanyika katika ofisi hiyo iliyopo Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma.

Mkaguzi wa Afya Mwandamizi-OSHA, Dkt. Edwin Senguo akiwasilisha mada kuhusu usalama na afya mahali pa kazi wakati wa mafunzo kwa watumishi wa ofisi hiyo yaliyolenga kuwajengea uwezo na kuimarisha utendaji kazi.

Sehemu ya Wakurugenzi na Watumishi wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI, wakifuatilia mafunzo ya kuwajengea uwezo na kuimarisha utendaji kazi yaliyofanyika katika ofisi hiyo iliyopo Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma.

Mtumishi wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bi. Flora Mnyandavile akiwasilisha hoja kwa Mkaguzi wa Afya Mwandamizi-OSHA, Dkt. Edwin Senguo (hayupo pichani) baada ya kuwasilisha mada kuhusu usalama na afya mahali pa kazi wakati wa mafunzo kwa watumishi wa ofisi hiyo yaliyolenga kuwajengea uwezo na kuimarisha utendaji kazi.

Sehemu ya Wakurugenzi Wasaidizi na Watumishi wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI, wakifuatilia mafunzo ya kuwajengea uwezo na kuimarisha utendaji kazi yaliyofanyika katika ofisi hiyo iliyopo Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma.

Na. Veronica Mwafisi-Dodoma

Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora imeahidi kuzingatia afya na usalama wa watumishi mahala pa kazi ili kuwa na nguvu kazi itakayowawezesha kufikia malengo la utoaji wa huduma bora kwa umma.

Kaimu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw. Xavier Daudi ameyasema hayo wakati akizungumza na watumishi wa ofisi yake katika eneo maalum la mafunzo kwa watumishi wake yanayofanyika kila siku ya Jumatatu Mtumba Jijini Dodoma.

“Ninamshukuru Mkaguzi wa Afya Mwandamizi kutoka OSHA, Dkt. Edwin Senguo kwa kuwasilisha mada kuhusu usalama na afya mahali pa kazi na sisi tunaendelea kuzingatia usalama na afya mahala pa kazi ikiwemo kuboresha miundombinu na mifumo ili kulinda afya za watumishi na kutoa huduma bora kwa wananchi.” amesema Bw. Daudi.

Aidha, amesisitiza watumishi kuendelea kutumia ngazi wakati wa kuingia ofisini kwa kuwa ni sehemu ya mazoezi yanayoimarisha afya.

Kwa upande wake Mkaguzi wa Afya Mwandamizi-OSHA, Dkt. Edwin Senguo amesema Wakala wa Usalama na Afya Mahala pa Kazi (OSHA) ni chombo cha kusimamia usalama na afya mahala pa kazi kwa kuhakikisha kwamba waajiri wote nchini wanaweka miundo na mifumo inayohakikisha usalama na afya mahala pa kazi vinalindwa.  

Dkt. Senguo amesisitiza Ofisi ya Rais-UTUMISHI kusimamia, kuwezesha, kuelimisha na kuhamasisha masuala ya Usalama na Afya Mahali pa Kazi kwa kuweka mifumo thabiti itakayo zuia ajali, magonjwa na vifo pamoja na uharibifu wa mali ili kupunguza gharama za uendeshaji na kukuza uchumi kwa maslahi ya Taifa.

About the author

mzalendo