Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akifungua rasmi Kongamano la Kodi na Uwekezaji la Mwaka 2025 linalofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam leo tarehe 15 Aprili 2025.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akisalimiana na Naibu Waziri wa Fedha Mhe. Hamad Hassan Chande wakati akiwasili katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam kwaajili ya kufungua Kongamano la Kodi na Uwekezaji la Mwaka 2025 leo tarehe 15 Aprili 2025.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akisalimiana na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe. Mhandisi. Zena Ahmed Said wakati akiwasili katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam kwaajili ya kufungua Kongamano la Kodi na Uwekezaji la Mwaka 2025 leo tarehe 15 Aprili 2025.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akiwa na Viongozi mbalimbali wakishiriki Kongamano la Kodi na Uwekezaji la Mwaka 2025 linalofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam. Tarehe 15 Aprili 2025.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akihutubia wakati akifungua Kongamano la Kodi na Uwekezaji la Mwaka 2025 linalofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam. Tarehe 15 Aprili 2025.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akiwa na Viongozi mbalimbali katika picha ya pamoja na wajumbe wa Tume ya Rais ya Maboresho ya Kodi mara baada ya ufunguzi wa Kongamano la Kodi na Uwekezaji la Mwaka 2025 linalofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam leo tarehe 15 Aprili 2025.
………
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango amesema Serikali ya Awamu ya Sita itaendelea kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji nchini ikiwemo kuimarisha hali ya ulinzi, amani na usalama na kuboresha mfumo wa viwango vya kodi.
Makamu wa Rais amesema hayo wakati akifungua Kongamano la Kodi na Uwekezaji la Mwaka 2025 linalofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam. Ametoa rai kwa washiriki wa Kongamano hilo kujielekeza katika kuibua mawazo na mikakati mipya itakayowezesha Taifa kuongeza makusanyo ya mapato ya ndani na hivyo kuiwezesha Serikali kutoa huduma bora kwa wananchi na kupunguza utegemezi kwa wahisani.
Aidha ametoa wito kwa wananchi kutumia vema fursa inayotolewa na Serikali kila mwaka kutoa maoni na kuwasilisha mapendekezo yao ya kuboresha sera za kodi na uwekezaji kwa kuchangia moja kwa moja katika jukwaa hilo au kupitia dirisha la kidigitali. Pia amewaagiza Mawaziri wa kila sekta kutoa maoni ya kuongeza mapato ya ndani katika sekta zao na kuhakikisha kuwa maoni na mapendekezo yatakayotolewa na wadau kwa njia mbalimbali yanafanyiwa kazi bila kudumaza ukuaji wa sekta husika.
Makamu wa Rais amesema zipo hatua mbalimbali zinazopaswa kutekelezwa zinazoweza kuongeza mapato ya ndani ikiwemo kuweka mkazo zaidi katika kuimarisha uwezo wa ukusanyaji na usimamizi wa mapato ya ndani, kuongeza jitihada katika kuboresha mfumo wa kodi ambao utahakikisha usawa na kuondokana na misamaha ya kodi isiyo na tija pamoja na kutoa vivutio vya kutosha kwa mawakala na taasisi za kukusanya kodi na kukabiliana na vitendo vya rushwa.
Makamu wa Rais ametaja hatua zingine za kutekelezwa ikiwemo kukuza matumizi ya TEHAMA katika ukusanyaji wa kodi na uwekaji wa akiba, kujenga kanzidata madhubuti ya taarifa za walipakodi na kufanya jitihada za kuongeza idadi ya walipa kodi kama njia ya kupunguza mzigo wa kodi, kubuni mbinu za kukabiliana na changamoto za kilojistiki na kisiasa katika utozaji wa kodi kutoka katika sekta isiyo rasmi, kuendelea kuboresha mazingira ya biashara ili kukuza uwekezaji pamoja na kuweka mfumo thabiti wa usimamizi, ufuatiliaji na upimaji kwa taasisi za kodi na zile za usimamizi.
Halikadhalika Makamu wa Rais amesema pamoja na jitihada kubwa zinazofanywa na Serikali ili kuongeza mapato, bado hali ya ulipaji kodi nchini inakabiliwa na changamoto mbalimbali hali inayopelekea ukuaji mdogo wa makusanyo ya ndani. Mathalan, uwiano wa mapato kwa Pato la Taifa umekuwa ukiongezeka kwa kasi ndogo katika kipindi cha zaidi ya miongo miwili kutoka 12.0% mwaka 2001/02 hadi 14.9% mwaka 2024/25.
Makamu wa Rais amelitaka Kongamano hilo kufanya tafakuri ya kina na kuainisha maboresho yanayohitajika kisera, kisheria, kikanuni na kiutaratibu ili kuwezesha uwekezaji na biashara na hivyo kuleta mageuzi makubwa katika mfumo wa kikodi na ukusanyaji wa mapato ya ndani.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Fedha na Mipango wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mhe. Saada Mkuya amesema Serikali ya Awamu ya Sita inatambua mchango wa Sekta Binafsi katika uwekezaji na hivyo imeendelea kuboresha mazingira ya uwekezaji na biashara nchini kupitia utekelezaji wa mpango wa kuboresha mazingira ya biashara nchini ili sekta binafsi iweze kushiriki kikamilifu katika kukuza uchumi wa Taifa.
Mhe. Mkuya ameongeza kwamba kupitia mpango huo, tozo na ada ambazo ni kero takribani 380 zimefutwa na baadhi zimepunguzwa. Amesema Serikali itaendelea kuhakikisha uhimilivu wa viashiria vya uchumi jumla, kuwa na sera za kodi ambazo zinatabirika na kuainisha tozo na ada mbalimbali zinazotozwa na Wizara na Mamlaka za udhibiti kwa lengo la kupunguza na kuimarisha usimamizi. Vilevile amesema mpango mwingine ni n matumizi ya TEHAMA ili kuweka urahisi wa kulipa kodi pamoja na kufanya biashara kwa ujumla.
Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini Angelina Ngalula amesema ni vema elimu sahihi kuendelea kutolewa kwa wafanyabiashara ili waweze kurasimisha biashara zao hali itakayopelekea waweze kupata faida za mikopo na ufadhili na hivyo serikali kuongeza wigo wa ukasanyaji kodi.
Ameongeza kwamba, jitihada lazima zifanyike kupitia vitengo vya utafiti vya Wizara kuhakikisha elimu inapatikana kwa wafanyabiashara ili kuondokana na idadi ndogo ya walipa kodi ambao ni milioni mbili waliopo hivi sasa. Na kupunguza gharama ya urasimishaji wa biashara ndogo ndogo.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Fedha na Mipango wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mhe. Saada Mkuya amesema Serikali ya Awamu ya Sita inatambua mchango wa Sekta Binafsi katika uwekezaji na hivyo imeendelea kuboresha mazingira ya uwekezaji na biashara nchini kupitia utekelezaji wa mpango wa kuboresha mazingira ya biashara nchini ili sekta binafsi iweze kushiriki kikamilifu katika kukuza uchumi wa Taifa.
Mhe. Mkuya ameongeza kwamba kupitia mpango huo, tozo na ada ambazo ni kero takribani 380 zimefutwa na baadhi zimepunguzwa. Amesema Serikali itaendelea kuhakikisha uhimilivu wa viashiria vya uchumi jumla, kuwa na sera za kodi ambazo zinatabirika na kuainisha tozo na ada mbalimbali zinazotozwa na Wizara na Mamlaka za udhibiti kwa lengo la kupunguza na kuimarisha usimamizi. Vilevile amesema mpango mwingine ni n matumizi ya TEHAMA ili kuweka urahisi wa kulipa kodi pamoja na kufanya biashara kwa ujumla.
Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini Angelina Ngalula amesema ni vema elimu sahihi kuendelea kutolewa kwa wafanyabiashara ili waweze kurasimisha biashara zao hali itakayopelekea waweze kupata faida za mikopo na ufadhili na hivyo serikali kuongeza wigo wa ukasanyaji kodi.
Ameongeza kwamba, jitihada lazima zifanyike kupitia vitengo vya utafiti vya Wizara kuhakikisha elimu inapatikana kwa wafanyabiashara ili kuondokana na idadi ndogo ya walipa kodi ambao ni milioni mbili waliopo hivi sasa. Na kupunguza gharama ya urasimishaji wa biashara ndogo ndogo
Kongamano hilo linashirikisha viongozi wa Serikali, wadau mbalimbali wa sekta binafsi, wafanyabiashara na wawekezaji. Kauli mbiu ya Kongamano hilo ni “ Kuongeza ukuzaji wa rasilimali za ndani kupitia kustawisha fursa za wananchi”