Featured Kitaifa

EWURA MWENYEJI MKUTANO WA MAMLAKA ZA UDHIBITI KUSINI MWA AFRIKA

Written by mzalendoeditor

 

Wajumbe wa Kamati ya Mawasiliano, Elimu kwa Umma na Huduma kwa Wateja katika picha ya pamoja mara baada ya kikao kilichofanyika Madnat AlBahr, Zanzibar.

Na.Mwandishi Wetu.

Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imekuwa mwenyeji wa vikao vya Kamati ndogo za Umoja wa Mamlaka za Udhibiti wa Sekta ya Nishati Kusini mwa Afrika (RERA) vilivyoanza rasmi leo, tarehe 23 Septemba 2024 visiwani Zanzibar.

Mamlaka za Udhibiti kutoka Angola, Botswana, Afrika Kusini, Namibia, Lesotho, Eswatini, Zambia, Malawi, Msumbiji, Zimbabwe na Tanzania zimeshiriki vikao hivyo.

Kwa upande wa Zanzibar, Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Maji na Nishati (ZURA) imeshiriki kama mtazamaji kwa kuwa bado haijawa mwanachama wa umoja huo.

Vikao hivyo vitakavyofanyika kwa awamu mbili, kati ya tarehe 23-27 Septemba, 2024, vinajadili pamoja na mambo mengine, namna ya kuboresha shughuli za udhibiti wa nishati katika maeneo ya fedha, rasilimali watu, huduma kwa wateja, habari, mawasiliano na teknolojia ya habari.

Masuala mengine ni kuhusu udhibiti kiufundi na kiuchumi ikijumuisha bei, tozo na viwango vya huduma kwenye sekta za umeme,

Wajumbe wa Kamati ya Fedha, Ukaguzi na Hesabu katika picha ya pamoja mara baada ya kikao kilichofanyika Madinat Al Bahr, Zanzibar.

 

Wajumbe wa Kamati ya Mawasiliano, Elimu kwa Umma na Huduma kwa Wateja katika picha ya pamoja mara baada ya kikao kilichofanyika Madnat AlBahr, Zanzibar.

Wajumbe wa Kamati mbalimbali wakishiriki vikao, Madnat Al Bahr, Zanzibar

About the author

mzalendoeditor