Featured Kitaifa

KASEKENYA AIPONGEZA TANROADS KWA VIFAA VYA KISASA VINAVYOTUMIKA KWENYE UJENZI WA BARABARA

Written by mzalendo

NAIBU  Waziri wa Ujenzi, Mhandisi Godfrey Kasekenya,akitoa maelezo mara baada yakukagua gari  alipotembelea banda la TANROADS kwenye Maonesho ya Kimataifa ya Wakulima Nanenane yanayofanyika katika  viwanja vya Nzuguni jijini Dodoma.

Na Alex Sonna-DODOMA
NAIBU  Waziri wa Ujenzi, Mhandisi Godfrey Kasekenya,amewataka wanaopewa dhamana ya kujenga miundombinu ya barabara kuzingatia ubora na thamani ya fedha.

Mha. Kasekenya, alisema hayo tarehe 8 Agosti, 2024 alipotembelea banda la maonesho ya Kimataifa ya Wakulima Nanenane la Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS), lililopo kwenye kwenye viwanja vya Nzuguni jijini Dodoma.

“Rai yangu kwa wanaopewa dhamana ya kutengeneza barabara wahakikishe kwamba wanasimamia ubora wa barabara na thamani ya barabara kwa kuwa wataalam tunao na vifaa vya kisasa tunavyo”, alisema Mha. Kasekenya.

Aidha, alisema hategemei kuona wataalamu walio na ujuzi na vifaa vya kisasa, lakini bado barabara zinaharibika kabla ya wakati.

Alisema, serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, imeendelea kuwekeza fedha nyingi kwenye ununuzi wa vifaa vya kisasa vya ujenzi wa barabara nchini.

“Serikali imewekeza kiasi kikubwa sana cha fedha ili kupata vifaa ambavyo vitasaidia kupata miundombinu bora ya barabara nchini” alisema Mha. Kasekenya.

 

Kadhalika, alisema TANROADS, hivi sasa inavifaa vya kisasa vinavyotumika kwenye ujenzi wa barabara ikiwemo vya kupima ubora wa udongo.

“Kuna mitambo ambayo inatumika kupima ubora wa udongo kuangalia ni udongo upi unafaa kwa ajili ya kubeba mizigo itakayokuwa inapita juu ya barabara,”…

Mha. Kasekenya ameongeza … “Na hapo pia wanamitambo ya inauwezo wa kuangalia kila tabaka la barabara linahitaji udongo upi na uwe na ubora upi kwa kila hatua inayofika na hata mitambo yao.inaweza kuonesha tabaka zote zikishakamilika kama zimejengwa kwa kiasi na kiwango kinachotakiwa” amesema Mha. Kasekenya.

Amesema, pia wanayomitambo inayoweza kupima kama kuna mpasuko ambayo maji yanaweza kupenya na kuharibu ubora wa barabara na kupunguza ubora wake.

Amesema pia kuna mtambo ambao unauwezo wa kupima barabara inayobonyea,unaoweza sababisha ajali au magari kutotembea katika hali ya usalama.

Hatahivyo alitoa wito kwa wakazi wa Dodoma na mikoa ya jirani kujitokeza kwa wingi kwenda kwenye banda la TANROADS, ili kujifunza teknolojia mbalimbali na kuona uwekezaji mkubwa uliofanywa na Serikali katika sekta ya ujenzi nchini.

NAIBU  Waziri wa Ujenzi, Mhandisi Godfrey Kasekenya,akipata maelezo kutoka kwa Mtalaam  wa Malighafi na Majenzi Barabara kutoka Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS),Kitengo cha Utafiti na Maendeleo,Mhandisi Christina Luhwaga, alipotembelea banda la TANROADS kwenye Maonesho ya Kimataifa ya Wakulima Nanenane yanayofanyika katika  viwanja vya Nzuguni jijini Dodoma.

NAIBU  Waziri wa Ujenzi, Mhandisi Godfrey Kasekenya,akitoa maelezo mara baada yakukagua gari  alipotembelea banda la TANROADS kwenye Maonesho ya Kimataifa ya Wakulima Nanenane yanayofanyika katika  viwanja vya Nzuguni jijini Dodoma.

NAIBU  Waziri wa Ujenzi, Mhandisi Godfrey Kasekenya,akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kutembele banda la  Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS),kwenye Maonesho ya Kimataifa ya Wakulima Nanenane yanayofanyika katika  viwanja vya Nzuguni jijini Dodoma.

NAIBU  Waziri wa Ujenzi, Mhandisi Godfrey Kasekenya,akiwa katika picha ya pamoja na Wafanyakazi mara baada ya kutembelea banda la Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS),kwenye Maonesho ya Kimataifa ya Wakulima Nanenane yanayofanyika katika  viwanja vya Nzuguni jijini Dodoma.

About the author

mzalendo