Featured Kitaifa

BALOZI WA DENMARK AMALIZA MUDA WAKE AMUAGA DKT. NCHEMBA

Written by mzalendo
Waziri wa Fedha, Mhe. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (Kulia), akiagana na Balozi wa Denmark nchini Tanzania aliyemaliza muda wake, Mhe. Mette Dissing-Spandet, baada ya kikao chao kilichofanyika katika Ofisi za Hazina Ndogo, jijini Dar es Salaam, ambapo ameiomba Denmark kuongeza ushirikiano katika sekta za nishati, maendeleo ya sekta ya fedha na kukuza uwekezaji, katika mpango wao mpya wa ushirikiano wa kimataifa unaoandaliwa na nchi hiyo.
 Waziri wa Fedha, Mhe. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), akizungumza wakati wa kikao na Balozi wa Denmark nchini Tanzania aliyemaliza muda wake, Mhe. Mette Dissing-Spandet (Hayupo pichani), katika Ofisi za Hazina Ndogo, jijini Dar es Salaam, ambapo ameiomba nchi hiyo kuongeza ushirikiano katika sekta za nishati, maendeleo ya sekta ya fedha na kukuza uwekezaji, katika mpango wao mpya wa ushirikiano wa kimataifa unaoandaliwa na nchi hiyo.
Balozi wa Denmark nchini Tanzania aliyemaliza muda wake, Mhe. Mette Dissing-Spandet, akizungumza wakati wa kikao na Waziri wa Fedha, Mhe. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (hayupo pichani), alipofika kumuaga katika Ofisi za Hazina Ndogo, jijini Dar es Salaam, ambapo Mhe. Dkt. Nchemba amewaomba kuongeza ushirikiano katika sekta za nishati, maendeleo ya sekta ya fedha na kukuza uwekezaji, katika mpango wao mpya wa ushirikiano wa kimataifa unaoandaliwa na Denmark.
 Ujumbe wa Tanzania (Kushoto), ukiongozwa na Waziri wa Fedha, Mhe. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) na Ujumbe wa Denmark ukiongozwa na Balozi wa Denmark nchini Tanzania aliyemaliza muda wake, Mhe. Mette Dissing-Spandet, wakiwa katika kikao chao kilichofanyika katika Ofisi za Hazina Ndogo, jijini Dar es Salaam, ambapo Dkt. Nchemba amewaomba kuongeza ushirikiano katika sekta za nishati, maendeleo ya sekta ya fedha na kukuza uwekezaji, katika mpango wao mpya wa ushirikiano wa kimataifa unaoandaliwa na Denmark.
 
 Balozi wa Denmark nchini Tanzania aliyemaliza muda wake, Mhe. Mette Dissing-Spandet (Kulia), akizungumza na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Bi. Amina Khamis Shaaban, kabla ya kuanza kikao chake na Waziri wa Fedha, Mhe. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (hayupo pichani), kilichofanyika katika Ofisi za Hazina Ndogo, jijini Dar es Salaam.
 
Waziri wa Fedha, Mhe. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (kulia), na Balozi wa Denmark nchini Tanzania aliyemaliza muda wake, Mhe. Mette Dissing-Spandet, baada ya kumalizika kwa kikao chao kilichofanyika katika Ofisi za Hazina Ndogo, jijini Dar es Salaam, ambapo Dkt. Nchemba amewaomba kuongeza ushirikiano katika sekta za nishati, maendeleo ya sekta ya fedha na kukuza uwekezaji, katika mpango wao mpya wa ushirikiano wa kimataifa unaoandaliwa na Denmark.
 Waziri wa Fedha, Mhe. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (katikati), Balozi wa Denmark nchini Tanzania aliyemaliza muda wake, Mhe. Mette Dissing-Spandet (wa tatu kushoto), Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Bi. Amina Khamis Shaaban (wa tatu kulia), wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Maafisa waandamizi wa Serikali ya Tanzania na Denmark, baada ya kikao chao kilichofanyika katika Ofisi za Hazina Ndogo, jijini Dar es Salaam, ambapo wamejadiliana masuala mbalimbali ikiwemo kuongeza ushirikiano kati ya nchi hizo mbili katika sekta za nishati, maendeleo ya sekta ya fedha na kukuza uwekezaji, katika mpango wao mpya wa ushirikiano wa kimataifa unaoandaliwa na Denmark.Mhe. Mette Dissing-Spandet alitumia kikao hicho kumuaga rasmi Mhe. Dkt. Nchemba baada ya kumaliza kipindi cha uwakilishi wake hapa nchini.
 (Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, WF, Dar es Salaam)
………
Na Benny Mwaipaja, Dar es Salaam
 
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), ameishauri Denmark kuongeza masuala ya ushirikiano katika sekta za nishati, maendeleo ya sekta ya fedha na kukuza uwekezaji katika mpango wao mpya wa ushirikiano wa kimataifa unaoandaliwa na nchi hiyo.
 
Dkt. Nchemba ametoa rai hiyo wakati akimuaga Balozi wa Denmark nchini Tanzania aliyemaliza muda wake, Mhe. Mette Dissing-Spandet, katika Ofisi za Hazina Ndogo, Jijini Dar es Salaam.
 
Katika kikao hicho, Dkt. Nchemba alimshukuru Balozi Dissing-Spandet kwa kufanikisha kusitishwa kwa uamuzi uliotaka kuchukuliwa na nchi yake wa kufunga ubalozi wake hapa nchini na kwa kuimarisha zaidi ushirikiano kati ya  Tanzania na Denmark.
 
Aidha, Dkt. Nchemba alisema kuwa mchango wa Denmark katika maendeleo ya nchi umekuwa mkubwa katika Nyanja mbalimbali ikiwemo ujenzi wa reli ya SGR, sekta ya afya, utawala bora, kukuza ajira, demokrasia, utawala wa sheria na haki za binadamu, miradi ambayo alisema inachangia kwa kiasi kikubwa kupunguza umasikini wa wananchi. 
 
Alimwomba Balozi huyo kuwa balozi mzuri wa Tanzania katika kuhamasisha kampuni za Denmark kuja kuwekeza nchini katika sekta mbalimbali za kiuchumi ikiwemo ujenzi wa viwanda vya kuzalisha mbolea na miradi ya nishati kwa njia ya upepo.
 
Kwa upande wake Balozi wa Denmark nchini Tanzania aliyemaliza muda wake, Mhe. Mette Dissing-Spandet, alisema kuwa anajivunia mafanikio makubwa yaliyopatikana katika kipindi cha uwakilishi wake hapa nchini ambapo ameshuhudia nchi ikipiga hatua kubwa kiuchumi na kijamii.
 
Aliahidi kuwa ataendelea kuwa balozi mzuri wa Tanzania ili kuvutia uwekezaji na kwamba kampuni nyingi za nchi yake zimeonesha nia ya kuwekeza hapa nchini.
 
Alisema kuwa alama kubwa anayoiacha ni pamoja na kuishawishi nchi yake kuachana na mpango wa kufunga shghuli za kibalozi hapa nchini na kwamba hatua hiyo itaiwezesha Denmark kujipanga upya na kuja na mpango mkubwa wa kushirikiana na Serikali katika kukuza maendeleo ya nchi.

About the author

mzalendo