Featured Kitaifa

RAIS SAMIA ATETA NA VIONGOZI WA KAMPUNI YA POSCO INTERNATIONAL YA KOREA

Written by mzalendo

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye mazungumzo na Ujumbe wa Kampuni ya Kimataifa ya POSCO International pamoja na viongozi wao Jijini Seoul, Jamhuri ya Korea tarehe 03 Juni, 2024. Kampuni hiyo imewekeza katika uchimbaji wa Madini ya Kinywe katika Mgodi wa Mahenge Graphite ambao ni mradi mkubwa wa pili Kidunia wa Madini hayo. Ujumbe huo Umeongozwa na Mwenyekiti na Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni hiyo Bw. Ghang In-Hwa, Rais wa POSCO Kye-in Lee pamoja na Wajumbe wengine wa Kampuni hiyo
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha ya pamoja na Mwenyekiti na Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya POSCO International inayowekeza kwenye Uchimbaji wa Mradi wa Madini wa Mgodi wa Mahenge Graphite ambao ni mradi mkubwa wa pili Kidunia wa Madini hayo. Ujumbe huo Umeongozwa na Mwenyekiti na Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni hiyo Bw. Ghang In-Hwa. Mazungumzo hayo yamefanyika Jijini Seoul Jamhuri ya Korea tarehe 03 Juni 2024.

About the author

mzalendo