Featured Michezo

WAZIRI NDUMBARO AMKARIBISHA WAZIRI WA MICHEZO IVORY COAST KWENYE DERBY YA KARIAKOO KUMUONA PACOME

Written by mzalendo

Na, Brown Jonas
Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro amekutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Michezo wa Ivory Coast  Mhe. Adjé Silas ambaye yupo nchini kwa ziara ya kikazi.Katika mazungumzo yao viongozi hao wamejadili  kuhusu ushirikiano wa nchi hizo kwenye Sekta ya michezo ambapo  Mhe. Ndumbaro amemualika  Mhe.Silas kushuhudia mechi ya Derby ya Kariakoo kati ya Yanga na Simba  itakayochezwa Aprili 20, 2024 katika Uwanja wa Benjamin Mkapa ili aone ladha ya mechi hiyo kubwa Afrika Mashariki pamoja na kuwaona wachezaji nyota wa timu hizo akiwemo mchezaji  Pacome Zouzoua wa Yanga ambaye ni raia wa Ivory Coast.

Mhe. Silas yupo nchini kwa ziara ya kikazi ambapo pia atashiriki hafla ya kuingia makubaliano ya ushirikiano kati ya Tanzania na Ivory Coast katika sekta ya michezo itakayofanyika Aprili 21, 2024 Jijini Dar Es Salaam

About the author

mzalendo