Featured Kitaifa

WANANCHI WATAKIWA KUFICHUA WATOTO WANAONYIMWA HAKI YA ELIMU

Written by mzalendo

Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Mwanaidi Ali Khamis akikata utepe kuzindua Taarifa ya Utekelezaji wa Azimio la Maputo Protocol uliofanyika jijini Dar Es Salaam.

Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Mwanaidi Ali Khamis akizungumza wakati wa uzinduzi wa Taarifa ya Utekelezaji wa Azimio la Maputo Protocol uliofanyika jijini Dar Es Salaam.

Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Mwanaidi Ali Khamis akikata utepe kuzindua Taarifa ya Utekelezaji wa Azimio la Maputo Protocol uliofanyika jijini Dar Es Salaam.

Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Mwanaidi Ali Khamis akionesha Taarifa ya Utekelezaji wa Azimio la Maputo Protocol mara baada ya uzinduzi wake uliofanyika jijini Dar Es Salaam.

Mkurugenzi wa Shirika la FAWE Tanzania Neema Kitainda Kitundu akieleza utekelezaji wa Azimio la Maputo Protocol wakati uzinduzi wa Taarifa hiyo uliofanyika jijini Dar Es Salaam.

Baadhi ya washiriki wakifuatilia hotuba na risala mbalimbali wakati wa uzinduzi wa Taarifa ya Utekelezaji wa Azimio la Maputo Protocol uliofanyanywa na Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Mwanaidi Ali Khamis jijini Dar Es Salaam.
Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini WMJJWM 
Na WMJJWM-Dar Es Salaam 
WANANCHI WATAKIWA KUFICHUA WATOTO WANAONYIMWA HAKI YA ELIMU 
Na WMJJWM-Dar Es Salaam 
Wananchi wamehimizwa kufichua familia ambazo bado zinawanyima watoto wa kike na kiume kupata elimu na badala yake kuwaozesha na kuwatumia katika shughuli za kiuchumi.
Wito huo umetolewa na Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Mwanaidi Ali Khamis wakati akizungumza katika uzinduzi wa Taarifa ya Utekelezaji wa Azimio la Maputo Protocol uliofanyika jijini Dar Es Salaam Aprili 18, 2023.
Naibu Waziri Mwanaidi amesema Tanzania ni miongoni mwa nchi 44 za Kiafrika zilizoridhia utekelezaji wa Azimio la Maputo Protocol la mwaka 2005, linalosisitiza kuhusu haki za wasichana na wanawake na kutoa msisitizo wa kutekeleza haki kwa wanawake, ikiwa ni pamoja na ushiriki katika siasa, usawa wa kijamii, kupata haki sawa ya elimu bora na kuondokana na mila na desturi zilizopitwa na wakati, mfano ukeketaji. 
“Kwa dhati ya moyo wangu, nitumie fursa hii kumpongeza Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuzingatia haki za mtoto hasa kwa hatua ya kuamua kuwarejesha shuleni watoto waliokatiza masomo ya elimu ya msingi na sekondari kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo utoro na kupata ujauzito.” ameeleza Naibu Waziri Mwanaidi 
“Napenda kutumia fursa hii kuwaomba kutomuacha nyuma mtoto wa kiume kwani dunia ya sasa imebadilika sana na watoto wa jinsi zote wapo hatarini kufanyiwa vitendo vya ukatili ukiwepo ukatili wa kunyimwa haki ya kupata elimu.” amesisitiza Naibu Waziri Mwanaidi 
Pia amesema anatambua kuwa Shirika la Wanawake Waelimishaji Afrika Tawi la Tanzania (FAWE Tanzania) kwa muda mrefu limekuwa mstari wa mbele katika kutetea haki ya elimu kwa mtoto wa kike bila kumuacha nyuma mtoto wa kiume na makundi maalum kwa ufadhili wa kutoka ECHIDNA Giving, kupitia Makao Makuu ya FAWE Afrika.
Aidha, Naibu Waziri Mwanaidi amesema moja ya sehemu ya utekelezaji wa azimio hilo la Maputo ni pamoja na kutoa elimu bila malipo kwa wanafunzi kuanzia elimu ya awali, msingi hadi kidato cha sita. 
Kwa upande wake Mwenyekiti Msaidizi wa Bodi ya FAWETZ  Cheka Omary Hussein amesema Taasisi hiyo kwa kushirikiana na wadau wengine wamejipanga ili kuhakikisha Taarifa ya Utekelezaji wa Taarifa ya Utekelezaji wa “Azimio la Maputo Protocol” nchini Tanzania inatekelezwa kwa Ushirikiano kati ya Serikali na Wadau wa Maendeleo.
 Utekelezaji wa Azimio hili utazingatia vipengele vya Ibara ya 5 inayohusu “kuondokana na mila potofu”, Ibara ya 6(b) inayohusu “ndoa za kulazimisha na ndoa za utotoni” na Ibara ya 12 inayohusu “haki ya kupata elimu na mafunzo” inaleta matokeo chanya katika maendeleo ya taifa.” amesema Cheka 
“Taarifa hiyo itawezesha kubainisha maeneo ambayo tumepata mafanikio kama nchi pamoja na maeneo tuliyopata changamoto na kuona kwa namna ya kushughulikia changamoto hizo.”amesisitiza Cheka

About the author

mzalendo