Featured Kitaifa

BURUNDI NA TANZANIA ZASAINI HATI YA MAKUBALIANO YA USHIRIKIANO KWENYE SEKTA YA MADINI

Written by mzalendoeditor

Bujumbura,Burundi.

Mawaziri wa Sekta ya Madini wa Burundi *Mh. Eng. Ibrahim Uwizeye* na Tanzania *Mh. Anthony Mavunde* leo wamesaini hati ya makubaliano ya kushirikiana kwenye sekta ya madini ili kukuza mchango wa sekta hii katika uchumi wa nchi mbili hizi.

Hafla ya kusaini makubaliano hayo imefanyika leo Jijini Bujumbura,Burundi na kuhudhuriwa na watalaamu wa nchi zote mbili.

Maeneo ya Ushirikiano yanajumuisha;

– Ujenzi wa Viwanda vya Uchenjuaji na Usafishaji wa Madini.
– ⁠Kubadilishana Uzoefu na utaalamu katika utafiti wa kina wa madini.

– ⁠Kuongeza thamani ya madini kwa kuzalisha bidhaa zitokanazo na madini.

– ⁠Kujenga uwezo wa kitaasisi na wataalamu wa pande zote mbili.

– ⁠Kusimamia sheria na taratibu za biashara ya madini inayohusisha pande zote mbili.

Akitoa maelezo ya awali Waziri wa Maji,Nishati na Madini wa Jamhuri ya Burundi *Mh. Eng. Ibrahim Uwizeye* amesema nchi ya Burundi
na Tanzania zimekuwa na urafiki wa muda mrefu na mahusiano mazuri,hivyo ni muhimu kutumia fursa hii kushirikiana kwenye sekta ya madini ili sekta hii itoe mchango unaostahili katika kukuza maendeleo ya Uchumi wa Burundi na Tanzania chini ya uongozi imara wa marais *Mh. Evariste Ndayishimiye*(_Burundi_) na *Mh. Dkt. Samia S. Hassan* (_Tanzania_)

Akizungumza katika hafla hiyo ,Waziri wa Madini wa Tanzania *Mh. Anthony Mavunde* amesema Tanzania ipo tayari kushirikiana na Burundi katika kuiimairisha na kuiboresha sekta ya madini ya nchi hizi mbili kwa kusimamia utekelezaji wa makubaliano ya ushirikiano yaliyofikiwa na kutumia fursa hii kuwaalika wachimbaji wa nickel,cobalt na copper kutumia huduma ya Kiwanda cha Usafishaji madini ambacho kitajengwa katika eneo la ulipokuwa Mgodi wa Buzwagi,Wilayani Kahama-Shinyanga.

About the author

mzalendoeditor