Featured Michezo

YANGA SC YAIVIMBIA MAMELODI SUNDOWS LIGI YA MABINGWA AFRIKA

Written by mzalendoeditor
MABINGWA wa Ligi Kuu Tanzania Bara timu ya Yanga SC imeshindwa kutamba kwenye uwanja wake wa nyumbani mara baada ya kulazimishwa sare 0_0  na Mamelodi Sundowns mchezo ulipigwa kwenye dimba la Benjamini Mkapa Jijini Dar es Salaam,.
Kipindi Cha kwanza Mamelodi waliweza kuutawala mchezo katika kipindi cha kwanza ambapo walitawala kwa asilimia 73% kwa 23% licha ya Yanga Sc kuwa na mashuti matatu yaliyolenga lango huku Mamelodi wakiwa wamepiga moja tu.
 
Kipindi cha pili Yanga walibadilika na kuonesha hali ya kulitaka bao la kuongoza bila mafanikio licha ya kupata nafasi za wazi nyingi.
 
Sifa za kipekee zimuendee mlinda mlango wa kimataifa wa Afrika Kusini, Ronwel Williams ambaye aliokoa hatari nyingi ambazo zilitengenezwa na Yanga Sc.

About the author

mzalendoeditor