Featured Michezo

BONANZA LA PASAKA LA WIZARA YA FEDHA LANOGA

Written by mzalendo
Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Rasilimali Watu wa Wizara ya Fedha, Bw. Lusius Mwenda (wapili kulia), akizungumza katika Bonanza la Pasaka lililofanyika katika viwanja vya Kilimani Jijini Dodoma, lililoandaliwa na Wizara ya Fedha kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais Fedha na Mipango Zanzibar, lengo likiwa ni kuimarisha uhusiano kati ya Wizara ya Fedha Tanzania Bara na Ofisi ya Rais Fedha na Mipango Zanzibar pamoja na Taasisi zake, Bonanza hilo linaambatana na matendo ya huruma yatakayofanyika tarehe 31/03/2024.
Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Rasilimali Watu wa Wizara ya Fedha, Bw. Lusius Mwenda, akikagua timu za mpira wa miguu zikihusisha wachezaji kutoka Wizara ya Fedha-Bara na wachezaji kutoka Ofisi ya Rais Fedha na Mipango Zanzibar, kabla ya kuanza kwa mchezo huo katika uwanja wa Kilimani Jijini Dodoma, lengo likiwa ni kuimarisha uhusiano kati ya Wizara ya Fedha-Bara na Ofisi ya Rais Fedha na Mipango Zanzibar pamoja na Taasisi zake.
Afisa Uendeshaji, Ofisi ya Rais Fedha na Mipango Zanzibar, Bw. Rajab Uweje, akizungumza, kwa niaba ya Mkurugenzi, Utumishi na Uendeshaji Ofisi ya Rais Fedha na Mipango Zanzibar Bw. Suleiman Mohammed Rashid, wakati wa kufungua Bonanza la Pasaka kwa niaba ya Mkurugenzi wa Utumishi, na Uendeshaji Ofisi ya Rais Fedha na Mipango Zanzibar, Bw. Suleiman Mohamed Rashid, lililofanyika katika viwanja vya Kilimani Jijini Dodoma, lengo likiwa ni kuimarisha uhusiano kati ya Wizara ya Fedha Tanzania Bara, Ofisi ya Rais Fedha na Mipango Zanzibar pamoja na Taasisi zake.
Afisa Uendeshaji, Ofisi ya Rais Fedha na Mipango Zanzibar, Bw. Rajab Uweje, akizungumza, na Afisa Usimamizi wa Fedha Mwandamizi, Wizara ya Fedha, Bw. Mgusi Musifa ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bonanza la Pasaka, mara baada ya mapumziko mafupi ya mchezo wa mpira wa miguu uliofanyika katika Uwanja wa Kilimani kati ya Wizara ya Fedha-Bara na Ofisi ya Rais Fedha na Mipango Zanzibar, katika mchezo huo timu hizo zimetoka suluhu.
Washiriki wa Mchezo wa Kuvuta Kamba wa Wizara ya Fedha kutoka Tanzania Bara, wakichuana kuvuta kamba dhidi ya washiriki kutoka Ofisi ya Rais Fedha na Mipango Zanzibar, (hawapo pichani), katika Bonanza la Pasaka lilofanyika katika viwanja vya Kilimani Jijini Dodoma huku Wizara ya Fedha Tanzania Bara ikiibuka mshindi wa shindano hilo, Lengo la Bonanza hilo ni kuimarisha uhusiano kati ya Wizara ya Fedha, Ofisi ya Rais Fedha na Mipango Zanzibar pamoja na Taasisi zake.
Baadhi ya washiriki waliohudhuria katika Bonanza la Pasaka liliofanyika katika Uwanja wa Kilimani, wakifuatilia michezo mbalimbali iliyokuwa inaendelea katika uwanja huo baina ya Wizara ya Fedha -Bara na Ofisi ya Rais Fedha na Mipango Zanzibar, ambapo michezo mbalimbali imechezwa ikiwemo, kuvuta kamba, mpira wa miguu na mpira wa kikapu.
Picha za matukio mbalimbali ya watumishi kutoka Wizara ya Fedha, Tanzania Bara na Ofisi ya Rais Fedha na Mipango Zanzibar, wakishiriki michezo ya kuvuta kamba na mpira wa miguu kwa wanaume, lengo likiwa ni kuimarisha uhusiano kati ya Wizara ya Fedha Tanzania Bara, Ofisi ya Rais Fedha na Mipango Zanzibar, pamoja na Taasisi zake, michezo hiyo imefanyika katika viwanja vya Kilimani jijini Dodoma.
 
(Picha na Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali, WF, Dodoma)
Na Chedaiwe Msuya na Asia Singano- WF- Dodoma
 
Wizara ya Fedha pamoja na Taasisi zake, Tanzania Bara na Ofisi ya Rais Fedha na Mipango zanzibar zimeendelea kuimarisha ushirikano wake kupitia njia mbalimbali ikiwemo michezo.
 
Akizungumza katika Bonanza la Pasaka lililofanyika katika Uwanja wa Kilimani jijini Dodoma, Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Rasilimali Watu wa Wizara ya Fedha, Bw. Lusius Mwenda, amesema michezo hiyo ni moja kati ya njia moja wapo ya kudumisha muungano kati ya Tanzania Bara na Zanzibar.
 
“Tupo hapa Kilimani kama wanamichezo kwa maana ya Ofisi ya Wizara ya Fedha, Tanzania Bara na wenzetu Ofisi ya Rais, wizara ya fedha kule Zanzibar, kila mwaka wakati wa Pasaka huwa tunakutana kama watumishi na kama wanamichezo kwa ajili ya kufanya Tamasha la Pasaka ambapo tunakuwa na michezo mbalimbali ikiwa ni pamoja na mpira wa miguu, kuvuta kamba, netiboli pia, kubwa sana katika mashindano haya ni ushirikiano kati ya sisi tuliopo Tanzania Bara na wenzetu walioko Tanzania Zanzibar’’ Alisema Bw. Mwenda.
 
Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi, Utumishi na Uendeshaji Ofisi ya Rais Fedha na Mipango Zanzibar, Bw. Suleiman Mohammed Rashid, mara baada ya kufungua Bonanza hilo, Afisa Uendeshaji, Ofisi ya Rais Fedha na Mipango Zanzibar, Bw. Rajab Uweje, ameshukuru Uongozi wa Wizara ya Fedha Tanzania Bara kwa kuendelea kushirikiana na Ofisi ya Rais Fedha na Mipango Zanzibar kuimarisha uhusiano kupitia Tamasha la Pasaka linalofanyika kila mwaka.
 
‘’Tunashirikiana katika masuala ya michezo kama haya kwa ajili ya kuimarisha udugu wetu na kuzidi kufahamiana katika masuala ya kazi, kwahiyo ni kitu kizuri ambacho tunakiendeleza tumekirithi kutoka kwa watangulizi wetu na kina manufaa makubwa sana kwetu sisi tunawashukuru viongozi wetu wa Wizara zetu hizi mbili kwa kuendelea kuimarisha mahusiano haya na yanatusaidia kwa kiasi kikubwa’’ alisema Bw. Uweje.
 
Kwa upande wa Mwenyekiti wa Bonanza la Pasaka ambaye pia ni Afisa Usimamizi wa Fedha Mwandamizi, Wizara ya Fedha, Bw. Mgusi Musifa, alisema kwa mwaka huu Kamati ya Maandalizi ya Tamasha hilo   imefanya maboresho katika Bonanza ikilinganishwa na miaka ya nyuma hususani katika mchezo wa mpira wa miguu kutokana na kuweka timu mbalimbali za nje mbali na timu ya Wizara ya Fedha, Tanzania Bara na Ofisi ya Rais Fedha na Mipango Zanzibar.
 
“Tukiongelea histori ya nyuma wakati huu tumeboresha kidogo, kwa sababu kawaida tulikuwa tukicheza sisi Hazina Bara na Hazina visiwani lakini leo tumekuwa na timu sita’’ aliongeza Bw. musifa.
 
Tamasha hili la Pasaka limekuwa likifanyika kwa zaidi ya miaka ishirini sasa na limekuwa likifanyika kwa kuunganisha pande zote mbili za Muungano kwa miaka yote hiyo. Na timu zilizoshiriki ni pamoja na timu ya Maveterani kutoka Bara na visiwani,Police FC, Hazina Sports club, GPSA, PSPTB, Area C na nyingine zao.

About the author

mzalendo