Featured Kitaifa

PROF. KIPANYULA ATAJA NGUZO KUJENGA NM- AIST BORA

Written by mzalendoeditor

Makamu Mkuu wa Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela Prof. Maulilio Kipanyula akizungumza wakati akifungua mafunzo ya viongozi wa Menejimenti na vikundi vya Watafiti yaliyoandaliwa na Taasisi hiyo kwa lengo la kuwajengea uwezo viongozi hao Mei 21, 2024 jijini Arusha.

Naibu Makamu Mkuu wa Taasisi Mipango,Fedha na Utawala Prof. Susan Augustino akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya viongozi wa Menejimenti na vikundi vya Watafiti yaliyoandaliwa na Taasisi hiyo kwa lengo la kuwajengea uwezo viongozi hao Mei 21, 2024 jijini Arusha.

Menejimenti na vikundi vya Watafiti kutoka Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela wakifuatilia masuala mbalimbali wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo yaliyoandaliwa na Taasisi hiyo Mei 21, 2024 jijini Arusha.

Viongozi wa Menejimenti ya Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela wakila kiapo cha Uadilifu wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo Menejimenti na vikundi vya Watafiti yaliyoandaliwa na Taasisi Mei 21, 2024 jijini Arusha.

………

Makamu Mkuu wa Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela Prof. Maulilio Kipanyula amesema uadilifu na kujitoa ni nguzo katika kutimiza majukumu ya uongozi na kujenga NM-AIST .

Ameyasema hayo Mei 21, 2024 Arusha wakati akifungua mafunzo ya siku tano ya Menejimenti na Watafit yaliyoandaliwa na Taasisi hiyo kwa lengo la kuwajengea uwezo viongozi hao.

Mafunzo hayo yanalenga kuongeza uelewa wa uwajibikaji na uadilifu katika utumishi wa umma, miiko ya uongozi, usimamizi wa fedha za umma ,uandaaji wa bajeti , matumizi ya fedha kudhibiti na kusimamia msongo wa mawazo pamoja na kusimamia afya ya akili.

Mafunzo hayo ya maadili kwa watumishi wa umma yanatolewa na Katibu Msaidizi – Ofisi ya Rais Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Ndg.Gerald A. Mwaitebele.

About the author

mzalendoeditor