Featured Kitaifa

RAFIKI DODOMA HOTEL KUZINDULIWA MACHI 9,MWAKA HUU

Written by mzalendoeditor

 

Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya uzinduzi wa Rafiki Dodoma Hotel Mhe.Peter Mavunde,akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo Machi 6,2024 jijini Dodoma kuelekea kwenye uzinduzi wa hotel hiyo ambayo itazinduliwa Machi 9,2024 jijini Dodoma na Naibu  Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko.

Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya uzinduzi wa Rafiki Dodoma Hotel Mhe.Peter Mavunde,akisisitiza jambo kwa  waandishi wa habari (hawapo pichani) leo Machi 6,2024 jijini Dodoma kuelekea kwenye uzinduzi wa hotel hiyo ambayo itazinduliwa Machi 9,2024 jijini Dodoma na Naibu  Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko.

Mkurugenzi Mtendaji wa Rafiki Dodoma Hotel Bw.Fladmiry Mallya,akizungumzia uzinduzi wa Rafiki Dodoma Hotel ambayo inatarajiwa kuzinduliwa  Machi 9,2024 jijini Dodoma na Naibu  Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko.

Msemaji wa Rafiki Dodoma Hotel Bw.Mpazi Zakayo,akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuelekea katika uzinduzi wa Rafiki Dodoma Hotel inayotarajiwa kuzinduliwaMachi 9,2024 jijini Dodoma na Naibu  Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko.

Muonekano wa Rafiki Dodoma Hotel ambayo itazinduliwa Machi 9,2024 na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko

Na. Alex Sonna-DODOMA

NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko, anatarajia kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa Rafiki Dodoma Hotel hafla itakayofanyika jijini Dodoma.

Akizungumza na Waandishi wa habari leo Machi 6,2024 Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya uzinduzi huo Mhe. Peter Mavunde, amesema kuwa uzinduzi huo utafanyika siku ya Jumamosi Machi 9,2024 jijini Dodoma ambapo hafla hiyo itafanyika jioni na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali.

Mhe. Mavunde amesema kuwa wananchi wa Dodoma wanastahili kujivunia maendeleo yanayopatikana katika awamu ya Sita chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika sekta ya uwekezaji.

”Uwekezaji huo ni juhudi kubwa zinazofanywa na Rais Samia ambapo amedhamira kuiweka Tanzani pamoja na Dodoma kuwa na mapinduzi ya viwanda ambavyo vimekuwa ni sehemu ya uwekezaji na hivyo kukuza uchumi hivyo kuzinduliwa kwa Hotel hii inatoa fursa za kimaendeleo kwa wananchi.”amesema Mhe. Mavunde

Aidha Mhe. Mavunde ameupongeza uongozi wa Rafiki Dodoma Hotel kwa kuendelea kuboresha mazingira katika maadhari mazuri ambapo itafanya wageni mbalimbali kuja kufanyia mikutano yao kwani ina kumbi nzuri hivyo jiji la Dodoma linajivunia kuwa na Hote hiyo.

”Naziomba Wizara ya Kisekta kuendelea kutangaza Vitutio vya utalii ili kuvutia wawekezaji kuja kuwekeza katika Mkoa wa Dodoma ili Mahotel yazidi kupata wageni wengi zaidi” amesema Mhe. Mavunde

Mhe. Mavunde ametoa wito kwa wawekezaji kote nchini kuja kuwekeza katika jiji la Dodoma kwani kwa sasa jiji hilo limezidi kuboresha mazingira pamoja na miundombinu katika hali ya kitaifa zaidi.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Rafiki Dodoma Hotel Bw. Fladmiry Mallya, amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuboresha mazingira mazuri kwa wawekezaji nchini.

”Tunaiomba Serikali yetu kuendelea kuboresha na kuweka mazingira wezeshi ya uwekezaji kwa wazawa ili kuzitangaza fursa za uwekezaji na vivutio vya utalii ambavyo vinachochea uwekezaji kuimarisha uchumi na ajira kwa watanzania”amesema Bw.Mallya

Amesema kuwa wanajivunia kuwa na Rais mwenye maono katika kuitangaza Tanzania katika Sekta ya uwekezaji sisi Rafiki Dodoma Hotel tumejipanga kutoa huduma bora kwa wageni wetu hivyo tunaomba Serikali izidi kuunga mkono katika uwekezaji huo.

Nae Meneja wa Rafiki Dodoma Hotel Bw. Mpazi Zakayo, amebainisha kuwa huduma zinazotolewa ni pamoja na vyumba vya kulala wageni, kumbi za mikutano, huduma za vinywaji, chakula, gym pamoja na huduma za kusafirisha wageni kwenda airport.

“Kwa ujumla tumeendelea kuboresha huduma zetu, kutokana na uhitaji mkubwa tumeongeza idadi ya vyumba vya kisasa wa ajili ya wageni wetu ikiwemo vyenye sifa ya _excutive suite_ , vyumba kwa ajili ya familia pamoja na kumbi za mikutano” amesema.Zakayo

About the author

mzalendoeditor