Kitaifa

DKT. BITEKO AMTEMBELEA RAIS WA ZANZIBAR KUHANI MSIBA WA MZEE ALI HASSAN MWINYI

Written by mzalendo

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amemtembelea na kumpa pole Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi nyumbani kwake Migombani, Unguja kufuatia kifo cha Baba yake mzazi, Hayati Mzee Ali Hassan aliyefariki dunia tarehe 29 Februari 2024 na kuzikwa tarehe 02 Machi 2024.

Kushoto kwa Mhe. Rais Dkt. Mwinyi ni Mkewe, Mama Mariam Mwinyi.

About the author

mzalendo