Mkuu wa kanisa la KKKT Tanzania Askofu Dkt. Alex Gehaz Malasusa akizungumza wakati wa ibada maalum ya Maombolezo na kuaga mwili wa Waziri Mkuu Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Edward Lowassa iliyofanyika katika Kanisa la kiinjili la kilutheri Tanzania (KKKT) Usharika wa Azania Front tarehe 14 Februari, 2024 Jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Dkt. Jim Yonazi akitoa maelekezo kwa timu ya Itifaki wakati wa maandalizi ya ibada maalum ya Maombolezo na kuaga Mwili wa Waziri Mkuu Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Edward Lowassa iliyofanyika katika Kanisa la KKKT Usharika wa Azania Front tarehe 14 Februari, 2024 Jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wanafamili ya Waziri Mkuu Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Edward Lowassa wakiwa ibadani wakati wa Maombolezo na kuaga Mwili wa Waziri Mkuu Mstaafu huyo iliyofanyika katika Kanisa la KKKT Usharika wa Azania Front tarehe 14 Februari, 2024 Jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya waombolezaji walioshiriki ibada maalumu ya maombolezo na kuaga mwili wa Waziri Mkuu Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Edward Lowassa iliyofanyika katika Kanisa la KKKT Usharika wa Azania Front tarehe 14 Februari, 2024 Jijini Dar es Salaam.
Mwili wa Waziri Mkuu Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Edward Lowassa ukiwasili katika Kanisa la KKKT Usharika wa Azania Front kwa ajili ya ibada maalum ya kuaga Jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya Viongozi wa Kanisa la KKKT Usharika wa Azania Front wakiingia kanisa kwa ajili ya ibada maalum ya Maombolezo na Kuaga Mwili wa Waziri Mkuu Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Edward Lowassa.
Baadhi ya Viongozi mbalilmbali walioshiriki katika ibada Maalum ya Maombolezo na Kuaga Mwili wa Waziri Mkuu Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Edward Lowassa.
(PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU)