Featured Kitaifa

BILIONI 2 KUTUMIKA KUBORESHA MIUNDOMBINU HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA WA SIMIYU

Written by mzalendoeditor

 

Naibu Waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel amesema Serikali imetenga kiasi cha shilingi bilioni mbili kwa mwaka wa fedha 2023/2024 kwa ajili ya kuanza ujenzi wa wodi za kulaza wagonjwa wa ndani pamoja na ujenzi wa uzio katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Simiyu.

Dkt. Mollel amesema hayo leo Jijini Dodoma wakati akijibu swali Namba 210 kwa niaba ya Waziri wa Afya, Mhe. Ummy Mwalimu lililoulizwa na Mbunge wa Viti Maalum, Mhe. Ester Lukago Midimu aliyetaka kujua ni lini Serikali itajenga uzio katika Hospitali ya Mkoa wa Simiyu?

Dkt.Mollel amesema kuwa Waziri wa Afya Mhe Ummy Mwalimu ashaelekeza Wizara kufanya tathimini ya Madaktari bingwa na Ubingwa bobezi ili kujua idadi yao katika maeneo waliopo ili kusambazwa nchini kulingana na mahitaji ya huduma za ubingwa bobezi katika mikoa.

About the author

mzalendoeditor