SIMBA SC ikiwa na Kocha Abdelhak Benchikha imepata ushindi wa kwanza baada ya kuichapa mabao 3_0 Kagera Sugar uliopigwa uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
Kipindi Cha kwanza Simba ilienda mapumziko ikiwa na bao moja lililofungwa na Saido Ntibazonkiza kwa penalti dakika ya 45.
Kipindi Cha pili Simba walipata mabao mawili kupitia kwa ( Sadio Kanoute dakika ya 75 na John Bocco dakika ya 90.
Kwa ushindu huo Simba imefikisha pointi 22 baada ya mechi tisa na kupanda hadi nafasi ya tatu ambapo imetanguliwa na kinara Azam na Yanga ya pili katika msimamo.