Featured Kitaifa

TAKUKURU DODOMA YAFUATILIA MIRADI 64 YENYE THAMANI ZAIDI YA SH.BILIONI 27.7

Written by mzalendo

 

MKUU wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa(TAKUKURU), Mkoa wa Dodoma,Bw.John Joseph wakati ,akitoa taarifa kwa  waandishi wa habari (hawapo pichani) leo Novemba 30,2023  jijini Dodoma kuhusu taarifa ya miezi mitatu za kazi za Taasisi hiyo.

Na.Alex Sonna-DODOMA

KATIKA kipindi cha Miezi mitatu kuanzia Julai  hadi Septemba mwaka huu Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa(TAKUKURU), Mkoa wa Dodoma imefuatilia miradi 64 yenye thamani ya zaidi ya sh. bilioni 27.7 katika sekta za elimu,ujenzi, afya,Maji na utawala,ustawi wa jamii na mifugo.

Hayo yamesemwa leo ,Novemba 30,2023 jijini Dodoma na Mkuu wa TAKUKURU  Mkoa wa Dodoma,Bw.John Joseph wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu taarifa ya miezi mitatu za kazi za Taasisi hiyo.

Amesema jumla ya miradi 51 ya elimu imefanyiwa ufuatiliaji, ujenzi mradi 1,utawala mradi 1,ustawi wa jamii mradi 1,mifugo miradi 2,Maji miradi 5,Afya Miradi 3.

Aidha Bw.Joseph amesema ufuatiliaji huo umefanyika sanjari na matumizi ya fedha za mpango wa maendeleo kwa Ustawi wa taifa na mapambano dhidi ya UVIKO-19 ambapo baadhi ya miradi yake imefuatiliwa.
“Katika ufuatiliaji huu wa miradi ya maendeleo tumebaini kuwepo kwa mapungufu kadhaa katika miradi 28 yenye thamani ya jumla ya shilingi bilioni tano milioni mia moja sitini na mbili laki mbili sabini na nne mia tano ishirini,”amesema Bw.Joseph
Amebainisha kuwa mapungulfu hayo ni pamoja na uekezaji wa majengo kwa kutumia mabati yaliyochini ya kiwppango (ubora hafifu) , baadhi ya majengo kuwa na nyufa nyingi, wazabuni kuliplwa fedha nyingi nje ya mkataba, kulipwa kabla ya kufikisha vifaa, kulipwa fedha nankuwasilisha vifaa pungufu.
Hata hivyo  ameongeza kuwa TAKUKURU imepokea jumla ya malalamiko 165 kati ya hayo 53 hayakuhusu rushwa hivyo walalamikaji 30 walielimishwa, 10 yamehamishiwa Jeshi la Polisi na 13 walalamikaji wake walishauriwa namna bora ya kutatua malalamiko waliyokuwa nayo.
Pia Bw.Joseph  ametaja vipaumbele vyao Kwa kipindi cha mwezi wa Oktabo mpka Disemba kuwa ni kufanya uchunguzi katika tuhuma zilizoainishwa katika taarifa ya mkaguzi na mdhibiti mkuu wa hesabu za serikali, malalamiko ya matumizi mabaya ya ofisi katika idaroa ya Ardhi katika Jiji la Dodoma na tuhuma nyingne kadri zitakavyo bainika.
Aidha  ametoa wito kwa wananchi kushiriki katika mapambano dhidi ya Rushwa kwani ni wajibu wa kikatiba ibara ya 9(H) na wakumbuke kuwa Rushwa ni ni adui wa taifa kama ilivyo ujinga, maradhi na umaskini.

About the author

mzalendo