Featured Kitaifa

WAZIRI GWAJIMA AMWAKILISHA RAIS SAMIA MKUTANO WA WANAUME KUTOKOMEZA UKATILI WA WANAWAKE

Written by mzalendoeditor

*PRETORIA – AFRIKA KUSINI*

*Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima* amemwakilisha *Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan* katika Mkutano wa Tatu wa Wanaume wa Umoja wa Afrika wa Wanaume Chanya katika Uongozi wa Kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Wasichana.

Lengo la mkutano huo uliofanyika Pretoria, Afrika ya Kusini tarehe 27-28 Novemba, 2023 ni kutathimini maendeleo ya wanaume kwenye uongozi chanya unaojielekeza kwenye Kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Wasichana.

Mada zilizowasilishwa na kujadiliwa ni pamoja na Hali halisi, Changamoto na shuhuda chanya kuhusu Ukatili dhidi ya Wanawake na Wasichana katika Kanda ya Afrika na Ripoti za Matokeo ya Mashauriano ya Wadau Mbalimbali.

Wakuu wa nchi wengine walioshiriki mkutano huo ni Rais wa Afrika Kusini *Mhe. Cyril Ramaphosa,* Rais wa Ethiopia *Mhe. Sahle- Work Zewde* na Rais wa Jamhuri ya Comoro *Mhe. Azali Assouman.*

Wengine ni Rais wa Zamani wa Jamhuri ya Mauritius *Ameenah Gurib-Fakim* na Rais wa zamani wa Jamhuri ya Afrika ya Kati *Mhe. Catherine Samba Panza* ambao wameshiriki kwa njia ya mtandao, pamoja na Marais wastaafu wa Liberia, viongozi mbalimbali kutoka nchi za Afrika na Mashirika ya Umoja wa Mataifa.

About the author

mzalendoeditor