Uncategorized

WAZIRI MCHENGERWA AELEKEZA UJENZI WA SHULE ZA WASICHANA ZA MIKOA UKAMILIKE DISEMBA 2023

Written by mzalendo

 

Naibu Katibu Mkuu (Elimu), Ofisi ya Rais-TAMISEMI Dkt. Charles Msonde akielekeza jambo wakati wa ziara yake ya kukagua ujenzi wa shule mpya ya sekondari ya wasichana ya mkoa wa Rukwa inayojengwa Laela katika Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga kupitia mradi wa SEQUIP.

Naibu Katibu Mkuu (Elimu), Ofisi ya Rais-TAMISEMI Dkt. Charles Msonde akisisitiza jambo wakati wa ziara yake ya kukagua ujenzi wa shule mpya ya sekondari ya wasichana ya mkoa wa Rukwa inayojengwa Laela katika Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga kupitia mradi wa SEQUIP.

Mafundi wakiendelea na ujenzi wa msingi wa moja ya jengo katika shule mpya ya sekondari ya wasichana ya mkoa wa Rukwa inayojengwa Laela katika Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga kupitia mradi wa SEQUIP.

Naibu Katibu Mkuu (Elimu), Ofisi ya Rais-TAMISEMI Dkt. Charles Msonde akiwa kwenye ukaguzi wa ujenzi wa shule mpya ya sekondari ya wasichana ya mkoa wa Rukwa inayojengwa Laela katika Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga kupitia mradi wa SEQUIP.

Mafundi wakiendelea wakiendelea na kazi ya ujenzi katika moja ya jengo la shule mpya ya sekondari ya wasichana ya mkoa wa Rukwa inayojengwa Laela katika Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga kupitia mradi wa SEQUIP.

Na: James Mwanamyoto-Laela

Naibu Katibu Mkuu (Elimu), Ofisi ya Rais-TAMISEMI Dkt. Charles Msonde amesema Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-TAMISEMI Mhe. Mohamed Mchengerwa ameelekeza ujenzi wa shule zote za wasichana za kitaifa za mikoa ukamilike ifakapo Disemba 2023 ili zianze kutumiwa na wanafunzi mwezi Januari. 

Dkt. Msonde amesema hayo leo, mara baada kukagua ujenzi wa shule mpya ya sekondari ya wasichana ya mkoa wa Rukwa inayojengwa Laela katika Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga kupitia mradi wa SEQUIP.

Dkt. Msonde amefafanua kuwa, majengo yote ya shule za mikoa za wasichana yanatakiwa kukamilika Disemba ili wanafunzi waliopangiwa katika shule hizo waanze masomo wakiwa katika miundombinu bora ya elimu.

“Mkurugenzi msimamieni mkandarasi na mhakikishe anaongeza mafundi wa kutosha ili ujenzi ukamilike kama alivyoelekeza Mheshimiwa Waziri,” Dkt. Msonde amesisitiza.

Dkt. Msonde amesema kuwa, shule hiyo ya wasichana ya mkoa wa Rukwa ndio shule pekee nchini ambayo ipo nyuma kiujenzi tofauti na shule nyingine ambazo kwa asilimia kubwa ujenzi wake umeshakamilika.

“Naona nyie hapa mpo nyuma kwasababu mmempa mkandarasi mmoja ajenge majengo yote wakati mlielekezwa kutumia force account ili muwe na wazabuni mbalimbali,” Dkt. Msonde amesema.

Ili kukamilisha ujenzi wa shule hiyo, Dkt. Msonde ameelekeza umeme uwekwe ili kazi ifanyike usiku na mchana na watendaji waliopewa dhamana ya usimamizi wawepo eneo la ujenzi kwa ajili ya kusimamia  na kufuatilia hatua zote za ujenzi.

Ameongeza kuwa, Serikali haitaki kusikia habari ya kutokamilika kwa ujenzi wa shule ambayo Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ameshatoa bilioni tatu ijengwe, kwani kitendo hicho kinaashiria kumkosea na kumuangusha katika utekelezaji wa nia yake ya kuboresha miundombinu ya elimu nchini. 

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-TAMISEMI Mhe. Mohamed Mchengerwa alimtuma Dkt. Msonde kukagua maendeleo ya ujenzi wa shule hiyo ya Sekondari ya wasichana ya Mkoa wa Rukwa kufuatia uwepo wa taarifa za kusuasua kwa ujenzi wake licha ya Serikali kupitia mradi wa SEQUIP kutoa bilioni tatu kuwezesha ujenzi.

About the author

mzalendo