Featured Michezo

TIMU YA WABUNGE YACHEZA MECHI YA KIRAFIKI NA TIMU YA MATI SUPER BRANDS LTD

Written by mzalendo

 Ferdinand Shayo ,Dodoma.

 
Timu ya mpira wa miguu ya Wabunge wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania imecheza mechi ya kirafiki na timu ya Wafanyakazi wa Kampuni ya Mati Super Brands Limited ambao ni wazalishaji wa vinywaji changamshi aina ya Strong Dry Gin,Tanzanite Premium Vodka,Sed Pineapple na Tai Original kwa lengo la kudumisha mahusiano mazuri kati ya Wabunge na makampuni ya Wawekezaji wazawa nchini.

 

 

Mkurugenzi wa Kampuni ya Mati Super Brands Limited David Mulokozi amewapongeza Wabunge kwa kushiriki katika mechi hiyo ya kirafiki iliyochezwa katika viwanja vya Kilimani vilivyopo Jijini Dodoma na kuonyesha uwezo mkubwa uwanjani Pamoja na wafanyakazi wa kampuni hiyo ambao wameshiriki mchezo huo.
 
“Kama unavyojua michezo ni afya ,michezo ni furaha lakini pia michezo inajenga urafiki Sisi kama Mati Super Brands Limited tunayofuraha sana kushiriki mechi hii tukiwa wadau wa maendeleo nchini na wadau wa michezo pia” Anaeleza David Mulokozi.
 
Mbunge wa Jimbo la Makete Festo Sanga amepongeza kampuni ya Mati Super Brands Limited na kuyataka makampuni mengine kuiga mfano na kuomba mechi za kirafiki na Wabunge kwani wao wako tayari wakati wowote na wanafanya mazoezi ya kutosha.

 

 

Kwa Upande wake Mbunge wa Viti Maalumu Asia Halamga amesema kampuni hiyo imekua mstari wa mbele katika ulipaji wa kodi na kutoa misaada kwa jamii inayowazunguka hivyo amempongeza Mkurugenzi wa Kampuni hiyo David Mulokozi kwa kutoa fursa za ajira kwa vijana .

 

 

About the author

mzalendo