Featured Kitaifa

JOKATE APOKELEWA KWA KISHINDO MAKAO MAKUU YA UWT TAIFA DODOMA

Written by mzalendoeditor

Katibu Mkuu wa Umoja wa Wanawake Tanzania Ndg.Jokate Mwegelo, akifurahi na Kucheza na kulakiwa na Wanachama na Viongozi wa UWT alipowasili Ofisi za Makao Makuu ya UWT leo Oktoba 12,2023 jijini Dodoma.

Na.Alex Sonna-DODOMA

KATIBU Mkuu wa Jumuiya ya Wanawake wa Chama cha Mapinduzi (UWT),Jokate Mwegelo ameahidi kuwa muadilifu,mtiifu na kusema  ameanza kazi rasmi ya kuhakikisha jumuiya hiyo inakuwa kimbilio na kivutio cha wanawake nchini.

Jokate ametoa ahadi hiyo leo Oktoba 12,2023 Jijini Dodoma baada ya kupokelewa na wanawake kwenye Makao Makuu ya Jumuiya hiyo.

Amesema kuwa  ameanza kazi rasmi ya kuhakikisha jumuiya hiyo inakuwa na umoja na ushirikiano pamoja na kuwaunganisha  wanawake wote watanzania ili  wajue UWT ndio kimbilio lao la kwanza.

“Naendelea kumuomba anipe akili ya kukitumikia hiki kiti cha Katibu  mkuu, Mwenyekiti wa CCM  Rais Samia ameonesha imani kwa kundi kubwa la vijana pia ameonesha imani kuwa kwa wanawake wa kitanzania,”amesema Jokate

“Niwahakikishie nitafanya kazi kwa uadilifu, utiifu mkubwa sana, imani ambayo nimekopwa nitailipa kwa Imani, najua kuna mipango kazi, mikakati imewekwa mimi nipo tayari kupokea maelekezo yako Mwenyekiti wangu kwa jinsi ambavyo unatamani hii jumuiya iende nitachapa kazi pamoja na wewe mwendo wako si wa mchezo.”

Aidha amewahimiza kushikamana, kupendana na kushirikiana ili kuonesha uhalisia nguvu ya wanawake wa kitanzania.

Kwa upande wake  Mwenyekiti wa UWT Taifa, Mary Chatanda,amewaasa wanawake kushirikiana pamoja katika kuhakikisha wanatafuta ushindi katika uchaguzi wa serikali za mitaa 2024 na uchaguzi mkuu 2025.

Awali Katibu Mkuu Mstaafu wa UWT, Dkt. Philis Nyimbi, ameshukuru kwa nafasi aliyopewa na Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais Samia kutumikia nafasi hiyo kwa zaidi ya miaka miwili na kwamba ujio wa Jokate utaongeza kasi ya mafaniko ya jumuiya hiyo.

Oktoba Mosi mwaka huu Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi CCM ilimteua Jokate Mwegelo kuwa Katibu Mkuu wa UWT akipokea kijiti kutoka kwa Dkt. Philis Nyimbi.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Wanawake Tanzania Ndg.Jokate Mwegelo akipeana Mkono na Bi Asha Iddi alipokwenda katika Soko la Machanga leo Oktoba 12,2023  Jijini Dodoma.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Wanawake Tanzania Ndg.Jokate Mwegelo akilakiwa na Wanachama na Viongozi wa UWT alipowasili Ofisi za Makao Makuu ya UWT leo Oktoba 12,2023 jijini Dodoma.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Wanawake Tanzania Ndg.Jokate Mwegelo akifurahi Jambo Katika tukio la Mapokezi yake lililofanyika Makao Makuu ya (UWT) leo Oktoba 12,2023 Jijini Dodoma.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Wanawake Tanzania Ndg.Jokate Mwegelo, akifurahi na Kucheza na kulakiwa na Wanachama na Viongozi wa UWT alipowasili Ofisi za Makao Makuu ya UWT leo Oktoba 12,2023 jijini Dodoma.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Wanawake Tanzania Ndg.Jokate Mwegelo, Akizungumza na Viongozi na Wanachama wa (UWT) alipowasili Ofisi za Makao Makuu ya UWT leo Oktoba 12,2023 Dodoma.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Wanawake Tanzania Ndg.Jokate Mwegelo, akikabidhiwa Rasmi Nyaraka za Ofisi na aliekua Katibu Mkuu wa Jumuiya Iyo Dkt. Philis Nyimbi,Makabidhiano hayo yameshuhudiwa na Mwenyekiti wa UWT Taifa Ndg. Mary Chatanda na Makamu Mwenyekiti wa UWT Ndg. Zainab Shomari wakiambatana na wajumbe wa Kamati ya Utekelezaji ya UWT Taifa
(Picha Zote na Fahadi Siraji)

About the author

mzalendoeditor