Featured Kitaifa

MRADI WA USAID TUWAJALI WATOTO WAZINDULIWA JIJINI DODOMA

Written by mzalendoeditor
Mkurugenzi wa Mafunzo na Maendeleo ya Sekta ya Afya  kutoka Wizara ya Afya Dk Saitore Laizer,akizindua Mradi wa USAID Tuwajali watoto  unaofadhiliwa na Mfuko wa dharura wa Rais wa Marekani wa Kupambana na Maambukizo ya VVU (PERFAR) kupitia Shirika la Marekani la Maendeleo la Kimataifa (USAID) kwa niaba ya Katibu Mkuu Wizara ya Afya leo Oktoba 12,2023 jijini Dodoma.
Na.Alex Sonna-DODOMA
Mradi wa USAID Tuwajali watoto  wenye lengo la kuwafikia watoto wengi zaidi walioathirika na Virusi vya Ukimwi na kuhakikisha wanatambuliwa na kupatiwa huduma umezinduliwa rasmi.
Mradi huo umefadhiliwa na Mfuko wa dharura wa Rais wa Marekani wa Kupambana na Maambukizo ya VVU (PERFAR) kupitia Shirika la Marekani la Maendeleo la Kimataifa (USAID).
Akizungumza leo Oktoba 12,2023 jijini Dodoma  wakati wa uzinduzi wa Mradi huo, Mkurugenzi Mtendaji wa Christian Social Services Commission (CSSC) Bw.Peter Maduki, amesema  mradi huo ni kwa ajili ya watoto wanaoishi na Virusi vya Ukimwi na una lengo la  kuboresha huduma ziweze kuhakikisha zinawafikia  watoto wengi na wanatambuliwa ambao wanaishi na Virusi.
Mradi huo una lengo pia la kuhakikisha watoto hao wanapata huduma bora katika maisha yao huku  wakiendelea kuishi na Virusi vya Ukimwi.
Amesema wanafanya kazi katika mikoa 11 nchini na  kwa kipekee na Hospitali ya kanda ya Mbeya kwa ajili ya kituo cha mfano ambacho kitakuwa na wataalamu na watatumika kuwafundisha wataalamu wengine.
”Mradi huo utagharimu Dola la Marekani 13.6 milioni ambao utatekelezwa kwa kipindi cha miaka mitano kuanzia 2023 hadi 2028 kwenye Mikoa ya Arusha, Dodoma, Kilimanjaro, Manyara, Singida, Iringa, Njombe, Lindi, Morogoro, Mtwara na Ruvuma”amesema Bw.Maduki 
Hata hivyo amesema kuwa watatekeleza jambo hili kwa kushirikiana na wadau wengine ambao wanatusaidia katika masuala ya kitaalamu,”amesema Bw. Maduki,
Kwa upande wake Mkurugenzi wa mradi wa USAID tuwajali watoto ambaye pia ni Daktari Bingwa wa watoto,kutoka Christian Social Services Commission (CSSC) Dk. Theopista  Masenge amesema malengo ya mradi huo ni kuwafuatilia wamama wajawazito wanaishi na VVU,watoto waliozaliwa na Mama wanaishi na VVU na watoto waliopata maambukizi au wanaoishi na maambukizi wenye umri wa miaka 0- 19.
Amesema wamefanikiwa baada ya kuona hakuna maambukizi kutoka kwa Mama kwenda kwa mtoto na watoto waliopata maambukizi hawafariki.
“Tunategemea kadiri wanavyotumia dawa vizuri wakasimamiwa basi Virusi vilivyokuwa kwenye mwili vinakuwa vimepungua kiasi kwamba haviruhusu kupata magonjwa nyemelezi,”amesema Dk.Theopista
Kuhusu wale wanaowaficha watoto alisema wamekuwa  wakifika katika nyumba  na kuzungumza na walezi na wazazi wenye watoto.
Amesema wana kampeni ya nyumba kwa nyumba kuhakikisha jamii imeelewa na tunawashikisha viongozi wa dini kwenye jambo hilo.
Naye,Mkurugenzi wa Huduma za Afya kutoka  Taaisis ya Christian Social Services Commission (CSSC), Dk Josephine Balati amesema mradi huo ni wa miaka mitano ambao umeanzia mwaka huu na  mpaka 2028.
Amesema mpaka sasa hapa nchini inakadiriwa kati ya watoto 90,000 mpaka 110,000 wanaishi na Maambukizi ya Virusi vya Ukimwi
Amesema tatizo kubwa lilopo ni asilimia 60 ya watoto hao wameweza kupimwa na kugundulika Wana matatizo.
“Bado Kuna wigo wa asilimia 40 ya watoto ambao bado hawajatambulika hali zao hata hao ambao wametambulika bado kuna changamoto katika matibabu yao hasa wale wa chini ya miaka 5 kwani wanategemea usimamizi wa wazazi ama walezi.
Dk Josephine amesema   watoto hao wanahaki ya kupata matibabu kamilifu ya Ukimwi na usimamizi wa lishe zao kwa ujumla.
Amesema lengo ni kuhakikisha watoto wote wanapimwa ili kujua afya zao.
“Tunatoa wito kwa Jamii kuangalia namna ya kuwasaidia watoto waweze kupata huduma,”amesema Dk Josephine.
Amesema familia nyingi zimekuwa na utaratibu wa kuwaficha watoto jambo ambalo sio zuri.
Awali  Mkurugenzi wa Mafunzo na Maendeleo ya Sekta ya Afya  kutoka Wizara ya Afya Dk Saitore Laizer amesema mradi huo uwaibue ile asilimia 40 ambayo bado haijulikani ilipo na haijaanza kutumia dawa ili kuliwezesha Taifa kuufuta ugonjwa wa Ukimwi ifikapo 2030.

Mkurugenzi wa Mafunzo na Maendeleo ya Sekta ya Afya  kutoka Wizara ya Afya Dk Saitore Laizer,akizungumza wakati wa uzinduzi wa Mradi wa USAID Tuwajali watoto  unaofadhiliwa na Mfuko wa dharura wa Rais wa Marekani wa Kupambana na Maambukizo ya VVU (PERFAR) kupitia Shirika la Marekani la Maendeleo la Kimataifa (USAID) kwa niaba ya Katibu Mkuu Wizara ya Afya leo Oktoba 12,2023 jijini Dodoma.

 Mkurugenzi Mtendaji wa Christian Social Services Commission (CSSC) Bw.Peter Maduki,akizungumza wakati wa uzinduzi wa Mradi wa USAID Tuwajali watoto  unaofadhiliwa na Mfuko wa dharura wa Rais wa Marekani wa Kupambana na Maambukizo ya VVU (PERFAR) kupitia Shirika la Marekani la Maendeleo la Kimataifa (USAID) leo Oktoba 12,2023 jijini Dodoma.
Mkurugenzi wa mradi wa USAID tuwajali watoto ambaye pia ni Daktari Bingwa wa watoto,kutoka Christian Social Services Commission (CSSC) Dk. Theopista  Masenge,akitoa taarifa ya mradi wakati wa uzinduzi huo wa  unaofadhiliwa na Mfuko wa dharura wa Rais wa Marekani wa Kupambana na Maambukizo ya VVU (PERFAR) kupitia Shirika la Marekani la Maendeleo la Kimataifa (USAID)leo Oktoba 12,2023 jijini Dodoma.
Mkurugenzi wa Huduma za Afya kutoka  Taaisis ya Christian Social Services Commission (CSSC), Dk Josephine Balati,akizungumza wakati wa uzinduzi wa mradi  huo  unaofadhiliwa na Mfuko wa dharura wa Rais wa Marekani wa Kupambana na Maambukizo ya VVU (PERFAR) kupitia Shirika la Marekani la Maendeleo la Kimataifa (USAID)leo Oktoba 12,2023 jijini Dodoma.
Sehemu ya washiriki wakimsikiliza Mkurugenzi wa Mafunzo na Maendeleo ya Sekta ya Afya  kutoka Wizara ya Afya Dk Saitore Laizer,(hayupo pichani)  wakati wa uzinduzi wa Mradi wa USAID Tuwajali watoto  unaofadhiliwa na Mfuko wa dharura wa Rais wa Marekani wa Kupambana na Maambukizo ya VVU (PERFAR) kupitia Shirika la Marekani la Maendeleo la Kimataifa (USAID) kwa niaba ya Katibu Mkuu Wizara ya Afya leo Oktoba 12,2023 jijini Dodoma.
Mkurugenzi wa Mafunzo na Maendeleo ya Sekta ya Afya  kutoka Wizara ya Afya Dk Saitore Laizer,akizindua Mradi wa USAID Tuwajali watoto  unaofadhiliwa na Mfuko wa dharura wa Rais wa Marekani wa Kupambana na Maambukizo ya VVU (PERFAR) kupitia Shirika la Marekani la Maendeleo la Kimataifa (USAID) kwa niaba ya Katibu Mkuu Wizara ya Afya leo Oktoba 12,2023 jijini Dodoma.

About the author

mzalendoeditor