Featured Kitaifa

MADAKTARI WAZAWA WAENDELEA KUPANDIKIZA FIGO MUHIMBILI, NJIA YA MATUNDU MADOGO KUTUMIKA

Written by mzalendoeditor


Madaktari wazawa Hospitali ya Taifa Muhimbili wanaendelea kufanya upasuaji wa kupandikiza figo ambapo wagonjwa 12 kuanzia leo watapata huduma hiyo sita kati yao watafanyiwa Upanga kwa njia ya kawaida na sita watafanyiwa wiki ijayo huko Mloganzila kupitia mfumo wa matundu madogo.

Akizungumza na Waandishi wa Habari Jijini Dar Es Salaam, Mkurugenzi wa Huduma za Tiba wa Hospitali hiyo Dkt. John Rwegasha amesema huu ni mwendelezo wa utoaji huduma za kibingwa nchini unaofanywa na madaktari wazawa ambao sasa wana ujuzi wa kutoa huduma hizo.

Dkt. Rwegasha amesema MNH inatekeleza Kwa vitendo azma ya Serikali ya kuhakikisha huduma za kibingwa na ubingwa bobezi zinaendelea kutokelewa nchini kutokana na uwekezaji mkubwa uliofanywa kwenye kusomesha watalaamu, ununuzi wa vifaa tiba na uwepo wa miundonbinu stahiki.

Tangu kuanzishwa huduma hii Hospitali ya Taifa Muhimbili imepandikiza wagonjwa 75 mwaka 2017.

About the author

mzalendoeditor