Featured Kitaifa

NAIBU WAZIRI MWANAIDI ATAKA KASI MIRADI CHUO CHA MAENDELEO YA JAMII BUHARE

Written by mzalendoeditor

Naibu Waziri Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Mwanaidi Ali Khamis akikagua mradi wa ujenzi wa jengo la kumbi la mihadhara katika Chuo cha Maendeleo ya Jamii Rungemba kilichopo Wilaya ya Musoma wakati wa ziara yake mkoani Mara 

Naibu Waziri Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Mwanaidi Ali Khamis akiangalia mashine ya kukandia unga wa ngano wakati akikagua shughuli za Kikundi cha Wajasirimali Queen Group katika  ziara yake mkoani Mara 

Naibu Waziri Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Mwanaidi Ali Khamis akisalimiana Mzee Meshack Magige, mmoja wa Wazee wanaoishi Makao ya Wazee ya Nyabange yaliyopo Wilaya ya Butiama wakati wa ziara yake mkoani Mara.

Naibu Waziri Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Mwanaidi Ali Khamis akicheza muziki na mmoja wa Mzee wanaoishi katika Makao ya Wazee ya Nyabange yaliyopo Wilaya ya Butiama wakati wa ziara yake mkoani Mara.

Naibu Waziri Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Mwanaidi Ali Khamis akitoa zawadi kwa Kituo cha kulea watoto cha Jipe Moyo kinachohudumia watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi na waliokimbia vitendo vya ukatili ikiwemo ukeketaji kilichopo Manispaa ya Musoma wakati wa ziara yake mkoani Mara 

Naibu Waziri Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Mwanaidi Ali Khamis akikagua mradi wa ujenzi wa jengo la kumbi la mihadhara katika Chuo cha Maendeleo ya Jamii Rungemba kilichopo Wilaya ya Musoma wakati wa ziara yake mkoani Mara 

Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe Mwanaidi Ali Khamis,akizungumza mara baada ya kutembelea na  kukagua ujenzi wa jengo la mihadhara Wilayani Musoma Mkoani Mara
(Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini WMJJWM) 
Na WMJJWM Musoma, Mara
Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe Mwanaidi Ali Khamis amekitaka Chuo cha Maendeleo ya Jamii Buhare kukamilisha mradi wa ujenzi wa jengo la mihadhara ili kuwezesha wanafunzi wengi wa fani ya Maendeleo ya Jamii kupata nafasi ya masomo.
Ameyasema hayo Wilayani Musoma Mkoani Mara Septemba 14, 2023 alipotembelea na kukagua ujenzi huo unaogharimu shillingi Millioni 50 mpaka kukamilika kwake.
Naibu Waziri Mwanaidi amesema, kukamilika kwa jengo hilo ni chachu ya kuongezeka kwa Maafisa Maendeleo ya Jamii ambao upatikanaji wake bado ni changamoto hasa kwa ngazi ya Kata na Mitaa.
Mwanaidi amesema, Serikali imetoa fedha ili kuboresha Vyuo vya Maendeleo ya Jamii vilivyo chini ya Wizara na kuvifanya  kuwa na mazingira bora  ya kufundishia na kujifunzia.
“Sisi kama Wizara tunaendelea kuboresha miundombinu katika Vyuo tunavyovisimamia ili tuwe na Vyuo vitakavyozalisha Wataalam wa Maendeleo ya Jamii wenye weledi na ufanisi” alisisitiza Naibu Waziri Mwanaidi.
Naye Mkuu wa Chuo cha Maendeleo ya Jamii Buhare Paschal Mahinyila amesema Chuo hicho kimefanikiwa kufanya mambo mbalimbali katika jamii ikiwemo tafiti ya namna ya kupambana na vitendo vya ukatili, kuhamasisha Jamii kwenye  masuala yahusuyo utunzaji mazingira, ujenzi wa Makazi bora na kushiriki shughuli za maendeleo katika maeneo yao.
Awali akisoma taarifa ya Mradi huo Makamu Mkuu wa Chuo cha Maendeleo ya Jamii Buhare Benard Ndiege amesema jengo hilo linajengwa kwa kutumia utaratibu wa kuwatumia wakandarasi wa ndani (force account) na litatatua changamoto za upungufu wa Majengo kwa ajili ya kumbi za mihadhara Chuoni hapo.
Katika hatua nyingine Naibu Waziri Mwanaidi ametembelea wazee wanaoishi katika Makazi ya Wazee Nyabange yaliyopo Manispaa ya Musoma na kuwaahidi kutatua changamoto ikiwemo uchakavu wa miundombinu iliyopo.
Vilevile Naibu Waziri Mwanaidi ametembelea Makao ya Watoto Jipe Moyo yanayotunza Watoto walio katika mazingira hatarishi na waliokimbia vitendo vya ukatili hasa ukeketaji huku akiwaasa wadau kuendelea kushirikiana na Serikali kuwasaidia watoto hasa wa kike walio katika mazingira magumu ili wapate sehemu salama ya kukaa na kujiendeleza.

About the author

mzalendoeditor