Featured Kitaifa

AMREF HEALTH AFRICA TANZANIA YAZINDUA MPANGO MKAKATI WAKE MPYA WA 2023-2030

Written by mzalendoeditor
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mkaazi wa AMREF Tanzania, Dkt. Florence Temu kuhusu historia ya AMREF nchini kabla ya kuzindua Mpango Mkakati wa AMREF Health Africa Tanzania wa Mwaka 2023-2030 kwenye hoteli ya Serena jijini Dar es salaam, Septemba 15, 2023.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mkaazi wa AMREF Tanzania, Dkt. Florence Temu kuhusu historia ya AMREF nchini kabla ya kuzindua Mpango Mkakati wa AMREF Health Africa Tanzania wa Mwaka 2023-2030 kwenye hoteli ya Serena jijini Dar es salaam, Septemba 15, 2023.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mkaazi wa AMREF Tanzania, Dkt. Florence Temu kuhusu historia ya AMREF nchini kabla ya kuzindua Mpango Mkakati wa AMREF Health Africa Tanzania wa Mwaka 2023-2030 kwenye hoteli ya Serena jijini Dar es salaam, Septemba 15, 2023.

 

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa (aliyevaa suti ya bluu) akikata utepe ishara ya kuzindua Mpango Mkakati wa AMREF Health Africa Tanzania wa Mwaka 2023-2030, Septemba 15, 2023. 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa (aliyevaa suti ya bluu) akikata utepe ishara ya kuzindua Mpango Mkakati wa AMREF Health Africa Tanzania wa Mwaka 2023-2030, Septemba 15, 2023. 

 

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mkurugenzi Mkaazi wa AMREF nchini, Dkt. Florence Temu kabla ya kuzindua Mpango Mkakati wa AMREF Health Africa Tanzania wa Mwaka 2023-2030 kwenye hoteli ya Serena jijini Dar es salaam, Septemba 15, 2023.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na viongozi alipowasili kwenye hoteli ya Serena jijini Dar es salaam kuzindua Mpango Mkakati wa AMREF Health Africa Tanzania wa Mwaka 2023-2030, Septemba 15, 2023. Kutoka kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya AMREF Tanzania Anthony Chamungwana, Waziri wa Afya wa Zanzibar, Nassor Mazrui , Mkurugenzi Mkaazi wa AMREF Tanzania, Dkt. Florence Temu na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Albert Chalamila.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akishiriki kuimba wimbo wa taifa kabla ya kuzindua Mpango Mkakati wa AMREF Health Africa Tanzania wa Mwaka 2023-2030 kwenye hoteli ya Serena jijini Dar es salaam, Septemba 15, 2023. Kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya AMREF Tanzania Anthony Chamungwana, Mkurugenzi Mkaazi wa AMREF Tanzania, Dkt. Florence Temu, Waziri wa Afya wa Zanzibar, Nassor Mazrui , na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Albert Chalamila. 
 
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI 
 
 Amref Health Africa Tanzania Yazindua Mpango Mkakati wake Mpya wa
2023-2030.
 
 Dar es Salaam, Tanzania – Septemba 15, 2023 – Shirika la Amref Health Africa, Tanzania
limezindua mpango mkakati wa kipindi cha mwaka 2023-2030.
 
 Uzinduzi huo ulihudhuriwa na Waziri Mkuu Mheshimiwa Kassim Majaliwa Majaliwa, na
unalenga kuunga mkono na kuboresha huduma bora za afya kwa Watanzania kupitia lengo lake
la kuendeleza na kuboresha huduma muhimu za afya zitakazoongozwa na jamii na watu wa
jamii hizo, huku ikizingatia kushughulikia Vibainishi vya afya vya kijamii (social determinants
of health). 
 
Kwa miaka thelathini na sita (36) sasa, Shirika la Amref Health Africa Tanzania limekuwa
likishirikiana na Serikali ya Tanzania hususani Wizara ya Afya na Ofisi ya Rais TAMISEMI pamoja
na wadau wengine katika kuboresha mifumo mbalimbali ya afya nchini.
Waziri Mkuu Mheshimiwa Kassim Majaliwa Majaliwa aliipongeza Amref Health Africa
Tanzania kwa kusaidia juhudi za serikali za kuhakikisha kuwa Watanzania wote wanapata
huduma bora za afya. 
 
“Nafurahi kwa kuwa Mpango mkakati huu mpya wa Amref Tanzania
unajikita katika kuboresha Afya ya msingi yaani Primary Health care kwa kupitia programu
zilizotajwa, huku ikiangazia vibainishi vya kijamii vya afya (Social determinants of health).
Naelewa kukabiliana na changamoto hizi inahitajika jitihada za wadau wa kada mbalimbali
kushirikiana ili kuleta tija,”
alisema Waziri Mkuu. 
 
Katika hotuba yake, Mkurugenzi Mkuu Mtendaji wa Amref Health Africa, Dkt. Githinji Gitahi
alisema, “Mnamo Machi 2023, Shirika la Amref Health Africa lilizindua mpango mkakati wa
miaka minane nchini Rwanda na maeneo ya kipaumblele yanalandana vyema na yale tajwa
Katika Mpango mkakati wa Amref Tanzania kwani kama nilivyosema changamoto za bara la
Afrika zinafanana kwa kiwango kikubwa.
Mpango mkakati huu umejikita kuleta majibu ya changamoto zinazotokana na viashiria vya
mabadiliko yanayotokea Barani Afrika na Ulimwenguni kwa ujumla ikichochewa na sera za Bara
la Afrika na Ulimwengu kwa ujumla ambazo zinaunda afya ya Waafrika.” 
 
Akizungumza na washiriki, Mkurugenzi Mkazi wa Amref Health Africa nchini Tanzania, Dkt.
Florence Temu alisema kuwa mpango mkakati huo utatoa mwelekeo kwa Amref Tanzania
katika kutekeleza majukumu yake ya msingi ya kuwekeza katika mifumo ya afya inayoongozwa
na jamii na inayolenga watu kwa ajili ya huduma endelevu za afya ya msingi. 
 
“Katika mpango mkakati wetu, ambao utadumu kwa miaka nane (2023-2030), tunajitahidi
kuhakikisha kuwa jamii nyingi zinafikia na kunufaika na huduma za afya ya msingi. Lengo letu
ni pamoja na kuwekeza katika Huduma ya Upatikanaji wa Huduma za Afya kwa Wote na
kushughulikia masuala ya kijamii yanayochangia kuenea kwa magonjwa yasiyoambukiza (NCDs)
na magonjwa mengine – ikiwa ni pamoja na magonjwa yanayohusiana na mabadiliko ya hali ya
hewa,”
alisema.
 
 “Zaidi ya hayo, tunalenga kuimarisha uwezo wa jamii zetu na mifumo ya afya kwa kushughulikia
athari za kiafya zinazotokana na mabadiliko ya hali ya hewa.  Kwa kujifunza kutokana na mlipuko
wa COVID-19, tunataka kuongeza uwezo wa sekta ya afya kukabiliana na milipuko. Aidha,
tutawawezesha wanawake na vijana kupitia elimu na hatua za kuboresha ubora wa maisha kwa
kutambua uhusiano muhimu kati ya ubora wa maisha na matokeo ya afya,”
aliongeza. 
 
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Amref Health Africa Tanzania,
Anthony Chamungwana alisisitiza dhamira ya Amref katika kusaidia juhudi za serikali katika
kukuza huduma za afya nchini. 
 
“Tutaendelea kufanya kazi kwa karibu na serikali na wadau
wengine ili kuhakikisha kuwa jamii zinapata huduma bora na nafuu za afya. Tutaendelea
kuwekeza katika huduma rafiki kwa watumiaji kulingana na miongozo ya nchi, na kuhakikisha
utekelezaji wa kiwango cha juu kutoka ngazi ya jamii hadi ngazi ya kitaifa,” alisema. 
 
Mpango mkakati huu wa 2023-2030 unatokana na uzoefu wa Amref Tanzania kutokana na
utekelezaji wa mikakati ya awali pamoja na vipaumbele na mwelekeo wa sasa wa kimataifa na
kitaifa. Kuongezeka kwa upatikanaji na matumizi ya huduma za Afya, kusaidia rasilimali watu
kwa afya, na kuhamasisha uwekezaji katika afya bado ni miongoni mwa maeneo ya
kipaumbele kwa Mkakati wa sasa. 
 
Aidha, mkakati huu unaweka mkazo zaidi katika kuimarisha
mifumo ya afya ya jamii kwa ajili ya kuboreshwa kwa upatikanaji, matumizi, na usimamizi wa
huduma katika ngazi ya jamii. Zaidi ya hayo, mkakati unalenga kushughulikia viashiria vya
kijamii vya afya, ikiwa ni pamoja na kuimarisha uwezo wa kukabiliana na mabadiliko ya hali ya
hewa na utayari wa vitisho vinavyoeza jitokeza. 
 
Amref Tanzania itaendelea kufanya kazi kwa ukaribu na wizara zote, mashirika ya serikali,
wafadhili, mashirika ya kijamii (CBOs), mashirika yasiyo ya kiserikali (NGOs), sekta binafsi, na
wanajamii. Kupitia utekelezaji wa mkakati huu, Amref Health Africa Tanzania inatarajia
kuchangia upatikanaji sawa na endelevu wa huduma bora za afya ya msingi (PHC) na hatimaye
kuchangia katika kufanikisha huduma ya afya kwa wote (UHC) nchini Tanzania.
 
 ################################################## 
 
 Kuhusu Amref Health Africa Tanzania 
 
Amref health Africa Tanzania ni shirika la kitanzania lilioandikishwa kisheria tangu mwaka wa
1987 na lina bodi ya wakurugenzi inayojitegemea na linaongozwa na watanzania. 
 
Amref Tanzania imekuwa mdau na mshirika mkubwa wa Serikali kwa kuwa na ushirikiano mzuri
na serikali hususani Wizara ya Afya na TAMISEMI katika kuboresha sera za afya kwa ujumla
wake, kutoa huduma za elimu ya afya, kuboresha huduma za tiba, kuratibu na kutengeneza
sera na miongozo mbalimbali ya kiafya.  Amref imewafikia watanzania wengi kupitia miradi ya
afya kwa afua mbalibambali inayotekelezwa katika mikoa mbalimbali ya Tanzania kama afya ya
mama na mtoto, vijana, afya ya uzazi, Kifua kikuu, Huduma za UKIMWI, UVIKO19, maji safi,
uboreshaji usafi wa mazingira na taka, kujengea uwezo wahudumu wa afya na mengine mengi. 
 
Kwa maelezo zaidi wasiliana na;
Eliminatha Paschal; Mkuu wa Mawasiliano na Mahusiano
Amref Health Africa in Tanzania 
 

About the author

mzalendoeditor