Featured Kitaifa

WAZIRI NDALICHAKO AHIMIZA USHIRIKIANO KUWAHUDUMIA WANANCHI

Written by mzalendoeditor

Na Mwandishi Wetu, Dodoma

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako amewataka watendaji wake kushirikiana kwa pamoja ili wananchi wapate huduma kwa wakati

Waziri Ndalichako ameyasema hayo wakati wa kikao kazi cha kujadili kazi za Ofisi hiyo pamoja na Taasisi zilizopo chini yake kilichofanyika Septemba 6, 2023 katika jengo la OSHA jijini Dodoma.

Aidha Prof. Ndalichako ameongeza kuwa kila mtendaji anajukumu la kutekeleza maagizo ya viongozi kwa haraka ili kuiwezesha serikali kufikia malengo na kuleta tija kwa wananchi.

Kwa upande wake Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu- Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhandisi Cyprian Luhemeja amemuhakikishia Waziri Ndalichako kuwa majukumu ya ofisi hiyo yatatekelezwa kwa kuzingatia Sheria, Taratibu na Kanuni.

Naye Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) Dkt. John Mduma akiongea kwa niaba ya Wakurugenzi Watendaji wa Taasisi zilizo chini ya Ofisi hiyo,  amebainisha kuwa wataendelea kutoa ushirikiano kwa Katibu Mkuu huyo mpya ili kufanikisha utekelezaji wa majukumu ya wizara pamoja na taasisi zake.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako akizungumza wakati wa kikao kazi cha kujadili kazi za Ofisi hiyo pamoja na Taasisi zilizopo chini yake kilichofanyika Septemba 6, 2023 katika jengo la OSHA jijini Dodoma. Kulia ni Katibu Mkuu Ofisi, ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhandisi Cyprian Luhemeja

Baadhi ya Viongozi wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu pamojan na Taasisi zilizo chini ya ofisi hiyo wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako (hayupo pichani)  wakati wa kikao hicho.

 Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhandisi Cyprian Luhemeja akieleza jambo wakati wa kikao hicho.

Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) Dkt. John Mduma akichangia jambo kwa niaba ya watendaji wa taasisi zilizo chini ya ofisi hiyo wakati wa kikao kazi hicho.

Kamishna wa kazi wa Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Suzan Mkangwa akiwasilisha taarifa za utekelezaji wa majuku wa Idara hiyo wakati wa kikao hicho.

Mkurugenzi wa Ajira na Ukuzaji Ujuzi wa Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Ally Msaki akiwasilisha taarifa za utekelezaji wa majuku wa Idara hiyo wakati wa kikao hicho.

About the author

mzalendoeditor