Featured Kitaifa

SERIKALI KUFANYA MABADILIKO KATIKA MASHIRIKA YA UMM

Written by mzalendoeditor

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza kwenye ufunguzi wa Kikao Kazi kwa Wenyeviti wa Bodi na Watendaji Wakuu wa Taasisi za Umma kilichoandaliwa na Ofisi ya Msajili wa Hazina kwa kushirikiana na Jukwaa la Wakuu wa Taasisi za Umma, kilichofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa AICC Jijini Arusha

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan na Viongozi mbalimbali wakati wa  wimbo wa Taifa na Afrika Mashariki alipowasili kwenye Ukumbi wa Mikutano katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano AICC Jijini Arusha kwa ajili ya kufungua Kikao Kazi kwa Wenyeviti na Watendaji Wakuu wa Taasisi za Umma 

       

– Advertisement –

Ad image

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza kwenye ufunguzi wa Kikao Kazi kwa Wenyeviti wa Bodi na Watendaji Wakuu wa Taasisi za Umma kilichoandaliwa na Ofisi ya Msajili wa Hazina kwa kushirikiana na Jukwaa la Wakuu wa Taasisi za Umma, kilichofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa AICC Jijini Arusha

           

Viongozi na Watendaji wa Taasisi mbalimbali wakisikiliza na kufuatilia kwa makini Hotuba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan alipokuwa akifungua Kikao Kazi kwa Wenyeviti wa Bodi na Watendaji Wakuu wa Taasisi za Umma kilichoandaliwa na Ofisi ya Msajili wa Hazina kwa kushirikiana na Jukwaa la Wakuu wa Taasisi za Umma, kilichofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa AICC Jijini Arusha .

                    

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akitoa Tuzo kwa baadhi ya Viongozi wa Taasisi na Kampuni zilizofanya vizuri kwenye kuchangia Maendeleo ya Serikali kwa Mwaka 2021/22, mara baada ya kufungua Kikao Kazi kwa Wenyeviti wa Bodi na Watendaji Wakuu wa Taasisi za Umma kilichoandaliwa na Ofisi ya Msajili wa Hazina kwa kushirikiana na Jukwaa la Wakuu wa Taasisi za Umma, kilichofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa AICC Jijini Arusha tarehe 19 Agosti, 2023

  

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipokea Tuzo kutoka kwa Waziri Mkuu Mhe. Kasssim Majaliwa kwa kutambua mchango wake mkubwa katika kuleta maendelea nchini , mara baada ya kufungua Kikao Kazi kwa Wenyeviti wa Bodi na Watendaji Wakuu wa Taasisi za Umma kilichoandaliwa na Ofisi ya Msajili wa Hazina kwa kushirikiana na Jukwaa la Wakuu wa Taasisi za Umma, kilichofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa AICC Jijini Arusha tarehe 19 Agosti, 2023

    

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha ya pamoja na Wenyeviti wa Bodi na Watendaji Wakuu wa Taasisi za Umma pamoja na Viongozi mbalimbali mara baada ya kufungua Kikao Kazi kwa Wenyeviti wa Bodi na Watendaji Wakuu wa Taasisi za Umma kilichoandaliwa na Ofisi ya Msajili wa Hazina kwa kushirikiana na Jukwaa la Wakuu wa Taasisi za Umma, kilichofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa AICC Jijini Arusha tarehe 19 Agosti, 2023

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amesema  ameridhia mapendekezo yaliyotolewa na Ofisi ya Rais – Mipango na Uwekezaji ya  kufuta na kuunganisha baadhi ya taasisi na mashirika ya umma.  

Rais Samia amesema hayo leo wakati akifungua kikao kazi cha Wenyeviti wa Bodi na  Watendaji Wakuu wa taasisi za umma kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa  kimataifa AICC. 

Aidha, Rais Samia ameiagiza ofisi hiyo kushirikiana na wizara za kisekta kuanza  mchakato wa kisera na kisheria kukamilisha mabadiliko hayo. 

Vile vile, Rais Samia amesema mabadiliko hayo yanatokana na kuingiliana na  kushabihiana kwa majukumu ya baadhi ya taasisi hivyo mpango wa kuziunganisha  zitaipunguzia serikali gharama za uendeshaji na kuongeza ufanisi na tija kiutendaji. 

Rais Samia pia ameitaka Ofisi ya Msajili wa Hazina kuhakikisha mpango huo  unafuata utaratibu na ushirikishwaji wa wadau wanaohusika, kulinda ajira na stahiki  za watumishi pamoja na mali za umma kipindi chote cha mpito. 

Rais Samia ameyataka mashirika ya umma kuvuka mipaka na kuwekeza nchi jirani  ili faida itakayopatikana itumike kuendesha mashirika hayo hapa nchini.  

Kwa upande mwingine Rais Samia amesema serikali inatarajia kuanza mchakato wa  kutunga sheria itakayobadilisha hadhi ya Ofisi ya Msajili wa Hazina kuwa Mamlaka  ya Uwekezaji wa Umma.  

About the author

mzalendoeditor