RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akishuhudia utiaji wa Saini ya Ushirikiano wa Miradi ya Sekta ya Afya baina ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China,wakisaini Waziri wa Afya Zanzibar Mhe. Nassor Ahmed Mazrui(kulia) na (kushoto) Balozi Mdogo wa China anayefanyia Kazi zake Zanzibar Mhe. Zhang Zhisheng, hafla hiyo iliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar leo 16-5-2023.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akisalimiana na Rais wa Taasisi ya “Chinese –African People’s Friendship Association (CAPFA)” Dr. Li Bin alipowasili Ikulu Jijini Zanzibar kwa ajili ya kushuhudia utiaji wa saini ya Ushirikiano wa Miradi ya Sekta ya Afya baina ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China, hafla hiyo iliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu Zanzibar leo 16-5-2023, na (kulia kwake) Balozi Mdogo wa China anayefanyia Kazi zake Zanzibar.Mhe. Zhang Zhisheng.
Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama Zanzibar na Viongozi wa Serikali, wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi, akizungumza wakati wa hafla ya utiaji wa Saini ya Ushirikiano wa Miradi ya Sekta ya Afya baina ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China, iliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar leo 16-5-2023.(Picha na Ikulu).