Featured Kitaifa

RC TANGA ATETA NA UONGOZI WA CHUO KIKUU MZUMBE

Written by mzalendoeditor

Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe, Prof. Mwegoha akikabidhi zawadi ya ukumbusho kwa Mkuu wa mkoa na Viongozi wengine wa mkoa huo.

Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo Prof. William Mwegoha akiwasilisha jambo kwa Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Mhe. Waziri Kindamba

 

Mhe. Kindamba akiwa pamoja na Katibu Tawala Mkoa wa Tanga Bi. Pili Mnyema (mwenye ushungi) na Mkuu wa Wilaya ya Mkinga (kulia) wakimsikiliza Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe

Viongozi wa chuo Kikuu Mzumbe wakiwa katika kikao cha Pamoja na Mkuu wa mkoa wa Tanga

Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe, Prof. Mwegoha akikabidhi zawadi ya ukumbusho kwa Mkuu wa mkoa na Viongozi wengine wa mkoa huo.

Na.Mwandishi Wetu

Mkuu wa mkoa wa Tanga, Mhe. Waziri Kindamba, amekutana na uongozi wa Chuo Kikuu Mzumbe ofisini kwake Leo, na kuwataka kuharakisha utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa Kampasi ya Tanga, unaokusudiwa kufanyika katika Wilaya ya Mkinga, kupitia Mradi wa Elimu ya Juu wa Mageuzi ua Kiuchumi(HEET), unaofadhiliwa na Benki ya Dunia.

Akielezea maendeleo ya mradi huo, Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo Prof. William Mwegoha amesema, tayari Chuo kimekamilisha Mpango wa Matumizi bora ya ardhi eneo lililotengwa kwa ujenzi, na kutangaza zabuni ya kumpata mkandarasi atakayehusika kufanya tathmini ya athari za kijamii na mazingira, ili ujenzi kuanza.

Ameahidi kuendelea kufuatilia kwa karibu utekelezaji wa ujenzi Pamoja na kuharakisha michakato ya ndani ili zoezi la ujenzi kuanza.

Mhe. Kindamba ameahidi ofisi Yake kuendelea kutoa ushirikiano wa karibu kwa chuo hicho katika kuhakikisha malengo ya mradi huo yanafikiwa na kuwanufaisha wananchi wa Tanga. Katika kikao hicho Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo aliambatana na Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Mipango, Fedha na Utawala Prof. Allen Mushi, Kaimu Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Taaluma, Utafiti na Huduma za Jamii Dr. Eliza Mwakasangula na Mratibu wa Ujenzi na miundombinu Bw. Prosper Leonard na Msaidizi wa Ujenzi Mhandisi Emmanuel Bura

About the author

mzalendoeditor