Featured Michezo

YANGA YAZIDI KUUKARIBIA UBINGWA WA 29,YAICHAPA GEITA GOLD

Written by mzalendoeditor

Na.Elick Mungele-Mzalendo blogs

MABINGWA Watetezi Yanga SC wameendelea kuukaribia Ubingwa wa 29 baada ya kutoka   nyuma na kuibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Geita Gold mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania bara uliopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.

Geita walikuwa wa kwanza kupata bao dakika ya 20 likifungwa na Elias Maguli na kuwapeleka mapumziko  wakiwa mbele ya bao hilo.

Kipindi cha Pili Yanga walifanya mabadiliko kwa wachezaji wake na walianza kuhesabu mabao yao kupitia kwa Washambuliaji wake Kennedy Musonda dakika ya 49 na Clement Mzize alipigiria msumari wa pili dakika ya 50.

Winga kutoka DRC Jesus Moloko alifunga bao la tatu mnamo dakika ya 70 Kwa ushindi huo Yanga SC wamefikisha Pointi 65 na kuendelea kuwacha kwa mbali watani zao Simba SC wenye Pointi 57 wakiwa nafasi ya pili.

Mchezo mwingine umepigwa uwanja wa CCM Mkwakwani wenyeji Coastal Union wameshindwa kung’ara katika uwanja wao baada ya kulazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na mchezo mwingine utapigwa muda mchache uwanja wa Jamhuri Dodoma wenyeji Dodoma jiji watacheza na Polisi Tanzania.

Ligi hiyo itaendelea kesho kwa mchezo mmoja matajiri wa Chamazi Azam FC watakuwa na kibarua kigumu dhidi ya Ihefu FC mchezo utakaopigwa Mbarali jijini Mbeya

About the author

mzalendoeditor