Featured Kitaifa

BALOZI KOMBO AWASILISHA HATI ZA UTAMBULISHO KWA RAIS WA JAMHURI YA MALTA

Written by mzalendoeditor

Rais wa Jamhuri ya Malta, Mheshimiwa Dkt. George Vella akipokea Hati za Utambulisho kutoka kwa Balozi wa Tanzania nchini Malta mwenye makazi yake Roma nchini Italia, Mhe. Mahmoud Thabit Kombo katika Ikulu ya Malt

Rais wa Jamhuri ya Malta, Mheshimiwa Dkt. George Vella akizungumza na Balozi wa Tanzania nchini Malta mwenye makazi yake Roma nchini Italia, Mhe. Mahmoud Thabit Kombo katika Ikulu ya Malta, mara baada ya Balozi Kombo kuwasilisha Hati za Utambulisho

Rais wa Jamhuri ya Malta, Mheshimiwa Dkt. George Vella katika picha ya pamoja na Balozi wa Tanzania nchini Malta mwenye makazi yake Roma nchini Italia, Mhe. Mahmoud Thabit Kombo katika Ikulu ya Malta

Balozi wa Tanzania nchini Malta mwenye makazi yake Roma nchini Italia, Mhe. Mahmoud Thabit Kombo amewasilisha Hati za Utambulisho kwa Rais wa Jamhuri ya Malta, Mheshimiwa Dkt. George Vella katika Ikulu ya Malta.

Baada ya kuwasilisha Hati za Utambulisho kwa Mhe. Rais Vella viongozi hao walizungumza ambapo pamoja na mambo mengine, mazungumzo hayo yaliakisi kuimarisha ushirikiano zaidi katika nyanja mbalimbali za kiuchumi na kisiasa na azma ya nchi ya Malta kuwa daraja baina ya Afrika na Umoja wa Ulaya.

Katika mazungumzo yao, viongozi hao walisisitiza suala la kuibua fursa zenye manufaa kwa pande zote mbili katika maeneo ya elimu, utalii, utamaduni, uvuvi, usafiri wa majini, biashara na uwekezaji.

Uhusiano wa kidiplomasia baina ya Tanzania na Malta ulianza mwaka 2015 na tangu wakati huo, juhudi za kukuza uhusiano huo zimekuwa zikifanyika kupitia sekta za elimu, utalii na usafiri wa anga; na kupitia katika majukwaa ya kimataifa ya Umoja wa Mataifa na Jumuiya ya Madola ambazo nchi zote mbili ni wanachama. 

About the author

mzalendoeditor