Uncategorized

NEEC YATOA MIKOPO KWA WATANZANIA TAKRIBANI MILIONI 9.8

Written by mzalendoeditor

KATIBU Mtendaji wa Baraza la Taifa la uwezeshaji wananchi kiuchumi (NEEC), Beng’i Issa,akizungumza na waandishi wa habari leo Februari 14,2023 jijini Dodoma wakati akitoa taarifa ya utekelezaji wa shughuli mbalimbali za Baraza hilo.

Na Alex Sonna-DODOMA

KATIBU Mtendaji wa Baraza la Taifa la uwezeshaji wananchi kiuchumi (NEEC), Beng’i Issa amesema katika kipindi cha mwaka jana watanzania takribani milioni 9.8 wamepatiwa mikopo ya kuwawezesha kujikwamua kiuchumi kupitia miradi mbalimbali.

Hayo ameyasema leo Februari 14,2023 jijini Dodoma wakati akitoa taarifa ya utekelezaji wa shughuli mbalimbali za Baraza hilo.

Amesema katika kipindi hicho mifuko ya uwezeshaji wananchi kiuchumi imetoa jumlaya Sh, trioni 5.6 ambapo wanawake walionufaika ni asilimia asilimia 53.

“Katika kipindi cha mwaka jana mifuko ya uwezeshaji wananchi kiuchumi ilitoa mikopo hiyo kwa watanzania takribani milioni 9.8 na kati yao wanawake ni asilimia 53 huku kiasi cha sh. trioni 5.6 zikitumika kuwezesha wananchi.”amesema Bi.Issa

Hata hivyo amesema kuwa  ukosefu wa elimu ya fedha na biashara umekuwa kikwazo kikubwa kwa wananchi kushindwa kufikia malengo yao ya kujikwamua kiuchumi.

“Elimu ya fedha na biashara bado ni kikwazo kikubwa kwa wananchi wetu kushindwa kujikwamua kiuchumi wengi wanakopa fedha lakini namna ya kuzitumia hawajui na kujikuta wakiingia katika mzigo wa madeni yasiyokuwa na tija kwao”amesema

Aidha amewataka Watanzania kuwa a na tabia ya kujiwekea akiba,ili waweze kuanzisha biashara zao hata bila kutegemea mikopo kutoka katika taasisi za kifedha kwa kuanza na kile kidogo walichojiwekea.

Pia amewataka wanachi kujenga tabia ya kuwa na bima za aina mbalimbali zitakazo wasaidia kulinda mali ambazo wamezitafuta kwa muda mrefu.

“Bima ni kitu cha muhimu sana tunapaswa kuwa na bima ya mali,afya,biasahara ili kulinda tulichokitafuta kwa muda mrefu leo hii unaweza kupoteza kila ulichokitafuta kwa jasho kutokana na kukosa bima”amesisitiza Issa

About the author

mzalendoeditor