Featured Kitaifa

WAZIRI BASHE ATETA NA WAZIRI WA KILIMO KUTOKA NCHINI KENYA

Written by mzalendoeditor

Waziri wa Kilimo, Mhe. Hussein Bashe leo Februari 3 amekutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Kilimo na Maendeleo ya Mifugo wa Jamhuri ya Kenya, Mhe. Mithika Linturi katika Ofisi za Wizara ya Kilimo, Kilimo IV, jijini Dodoma.

Mawaziri hao wawili wamekubaliana kuimarisha ushirikiano katika sekta ya kilimo kwa kubadilishana ujuzi katika tafiti za kilimo ili kuongeza upatikanaji wa chakula katika Jumuiya ya Afrika Mashariki.

About the author

mzalendoeditor