Featured Kitaifa

WAZIRI GWAJIMA AZIKUMBUSHA NGOs KUFUATA MISINGI YA KATIBA, SHERIA NA KANUNI

Written by mzalendoeditor

 

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Dorothy Gwajima akizungumza na Wajumbe wa Bodi ya 5 ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali wakati wa uzinduzi wa Bodi hiyo iliyofanyika leo Januari 18,2023  jijini Dodoma.

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Dorothy Gwajima akimkabidhi Mwenyekiti Mpya wa Bodi ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Bi. Mwantum Mahiza, vitendea kazi ikiwa ni ishara ya uzinduzi wa Bodi hiyo uliofanyika jijini Dodoma Januari 18, 2023

Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Mwanaidi Ali Khamis akizungumza na wajumbe wa Bodi ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali wakati wa uzinduzi wa  Bodi hiyo Januari 18, 2023.

Mbunge wa viti maalum kutoka Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Mhe. Neema Lugangira akieleza jambo wakati wa Uzinduzi wa Bodi ya 5 ya Mashirika Yasiyo Ya Kiserikali uliofanyika jijini Dodoma Januari 18, 2023.

Mwenyekiti Mpya wa Bodi ya Mashirika Yasiyo Ya Kiserikali Bi Mwantumu Mahiza akizungumza baada ya Uzinduzi wa Bodi ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Januari 18, 2023.

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Dorothy Gwajima katika picha ya pamoja na wajumbe wa Bodi ya 5 ya NGOs baada ya kuizindua jijini Dodoma Januari 18, 2023
Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini WMJJM
…………………………….
Na WMJJWM, Dodoma
Mashirika Yasiyo ya Kiserikali (NGOs) yametakiwa kufuata misingi ya katiba, sheria na kanuni zilizowekwa katika utekelezaji wa majukumu Yao.
Akizindua Bodi ya 5 ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali, jijini Dodoma leo Januari 18, 2023, Waziri wa Maendeleo ya Jamii,Jinsia ,Wanawake na  Makundi Maalum Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima ameitaka Bodi hiyo kusimamia vema uendeshaji wa Mashirika hayo kuanzia ngazi za chini na kufungamanisha taarifa za utekelezaji wa NGO na taarifa za serikali zinazowasilishwa ngazi zote Ili jamii ione tija ya utekelezaji wa NGO na kushirikiana zaidi.
Amesema NGO’s ni wajumbe wa kamati mbalimbali zinazohusika kusukuma ajenda za serikali mfano katika kupambana kutokomeza ukatili wa kijinsia na kwa watoto hivyo, NGO zina haki ya kupaza sauti kwenye Bodi ya NGO iwapo hakuna ufanisi wa kamati na NGO zipo Ili kusaidia. Lengo ni wadau kuisadia serikali na Serikali kuziwezesha NGO kutimiza wajibu wao na wananchi kunufaika.
“Kuna baadhi ya Mashirika yanaendesha shughuli zao kinyume na Sheria za nchi, hivyo mje na njia ya kupata Taarifa. NGOs ziko nyingi zinazofanya kazi Nzuri lakini zipo ambazo zinafanya mambo ambayo hayaendani na Tamaduni zetu, mchukue hatua” Alisisitiza Dkt Gwajima.
Aidha Dkt Gwajima ameipongeza Bodi iliyopita na kuwaagiza kuendelea kutoa ushirikiano  kwa  wajumbe wa Bodi mpya na kumpongeza Mwenyekiti Bi Mwantumu na Wajumbe wote.
Kwa upande wake, Mwenyekiti mpya wa Bodi Bi Mwantumu Mahiza amemshukuru Raise Samia Suluhi Hassan kwa kumuamini kusimamia chombo hicho muhimu na kuwasisitiza Wajumbe wateule kujipanga kuhakikisha NGOs zinafanya kazi inavyoonekana.
Bi. Mahiza amesema atasimamia Bodi kuhakikisha NGOs zinafanya kazi kwa kufuata kanuni na sheria za nchi kwa kuona kila shirika linafanya nini.
“Umuhimu wa chombo hiki ni kuhakikisha Mashirika yanafanya kazi zinazoonekana, lakini kuna uharaka unahitajika wa sisi kama Bodi kupitia sheria, sera na kanuni ili tuone kama zinaendana na matakwa ya nchi na wakati tulio nao” amesema Mwantum.
Naye Mbunge wa viti maalum mwakilishi wa NGOs Mhe. Neema Lugangira ameiomba Serikali kupitia Bodi hiyo kuangalia baadhi ya Changamoto ambazo zimeendelea kufanya Bodi kushindwa kufanya kazi inavyotakiwa ikiwemo ushirikishwaji kwenye vikao vya kisekta.
“Changamoto nyingine ni Upatikanaji wa Vibali kwa muda  ili kusaidia Mashirika kuweza kufanyia kazi  zao za kuwafikia Wananchi kwa uharaka zaidi”Alisema  Neema Lugangira.
Uzinduzi wa Bodi hiyo umehudhuriwa pia na Naibu Waziri Mhe. Mwanaidi Ali Khamis na Katibu Mkuu Dkt. Zainab Chaula.

About the author

mzalendoeditor