Featured Kimataifa

MAJALIWA AMWAKILISHA RAIS SAMIA KATIKA MAADHIMISHO YA MIAKA 75 YA MSIKITI WA CHUO KIKUU CHA MAKERERE NCHINI UGANDA

Written by mzalendoeditor

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Waziri anayeshugulikia Masuala ya jiji la Kampala  (Minister for Kampala City  and Metropolitan Affairs), Hajjat  Misi Kibanda wakati alipomwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan  katika  maadhimisho ya  miaka 75 tangu ulipojengwa  msikiti wa kwanza katika Chuo Kikuu cha Makerere Kampala, Uganda, Desemba 17, 2022. Msikiti huo ulifunguliwa na Mwana wa Mfalme Abdullah wa Zanzibar 1948. 

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza wakati alipomwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan   katika maadhimisho ya  miaka 75 tangu ulipojengwa  msikiti wa kwanza katika Chuo Kikuu cha Makerere Kampala, Uganda, Desemba 17, 2022. Msikiti huo ulifunguliwa na Mwana wa Mfalme Abdullah wa Zanzibar 1948.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wakati alipomwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan   katika  maadhimisho ya  miaka 75 tangu ulipojengwa  msikiti wa kwanza katika Chuo Kikuu cha Makerere Kampala, Uganda, Desemba 17, 2022. Msikiti huo ulifunguliwa na Mwana wa Mfalme Abdullah wa Zanzibar 1948.

Msikiti wa kwanza katika Chuo Kikuu cha Makerere nchini Uganda ulifunguliwa na Mwana wa Mfalme Abdullah wa Zanzibar 1948. Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alimwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika maadhimisho ya miaka 75 tangu ulipojengwa yalyofanyika Kampala,

  

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki, Balozi Mbarouk Nassoro Mbarouk (kulia) wakiwa katika picha ya pamoja na wanachuo Watanzania wanaosoma katika Chuo Kikuu cha Makerere nchini Uganda wakati alipomwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan   katika  maadhimisho ya  miaka 75 tangu ulipojengwa  msikiti wa kwanza katika Chuo Kikuu hicho , Desemba 17, 2022. Msikiti huo ulifunguliwa na Mwana wa Mfalme Abdullah wa Zanzibar 1948.

(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

………………………..

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema kuwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania itaendelea kuenzi uhusiano wa kidini na kiutamaduni kati yake na Uganda.

Amesema hayo leo Jumamosi (Disemba 17, 2022) alipomwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika maadhimisho ya miaka 75 tangu ulipojengwa msikiti wa kwanza katika Chuo Kikuu cha Makarere kilichopo Kampala nchini Uganda. Msikiti huo ulifunguliwa na Mwanamfalme Abdullah wa Zanzibar mwaka 1948

Mheshimiwa Majaliwa amesema kuwa  ujenzi wa msikiti huo umekuwa ni chachu ya kuimarisha mahusiano ya enzi kati ya wananchi wa Uganda, Zanzibar na iliyokuwa Tanganyika.

“Nyote mtakubaliana nami kwamba uwepo wetu hapa ni ishara tosha ya kutambua umuhimu na mchango wa tukio hili la kihistoria katika kukuza mahusiano ya watu wetu hususan ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki”

Aidha, Waziri Mkuu ameishukuru Serikali ya Uganda na Chuo Kikuu cha Makerere katika kuusimamia Msikiti huo sambamba na kuruhusu Waislamu wa maeneo ya jirani kuutumia kwa ajili ya kuabudu

Katika hatua nyingine, Mheshimiwa Majaliwa ametoa  rai kwa viongozi wa dini kuendelea kukemea mmomonyoko mkubwa wa maadili ambao umeshika hatamu.

“Katika hili ningeomba turejee maneno ya maneno ya Mwenyezi Mungu Mtukufu katika Qur‘an tukufu Sura ya 33 Ayah 21 (Quran 33:21) kwamba “Hakika ninyi mnacho kiigizo chema kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu”.

Ameongeza kuwa taasisi za elimu, jumuiya za dini, viongozi wa dini na viongozi wa umma wanao wajibu wa kuilea jamii kwa kutoa elimu sahihi ya mazingira sambamba na mafundisho sahihi na endelevu ya dini ili kuiwezesha kutambua na kufuata yote yaliyo mema kama tulivyo amrishwa na Mwenyezi Mungu na kuacha kabisa yote mabaya yanayomchukiza Mwenyezi Mungu.

“Nitumie fursa hii kuwaomba viongozi wa Jumuiya kuongeza juhudi katika kutoa mafunzo ya dini ili kuijengea Jamii hofu ya Mwenyezi Mungu dhidi ya maovu na hivyo, kupunguza au kuondoa kabisa mmomonyoko wa maadili tunaoushuhudia sasa”

Awali Akizungumza katika maadhimisho hayo Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Makerere alisema kuwa Prof. Umaru Kakumba alisema kuwa ujenzi wa msikiti huo ulilenga kujenga maadili mema miongoni mwa wanachuo .

About the author

mzalendoeditor