Featured Kitaifa

MWENYEKITI CCM JUMUIYA YA WAZAZI DAR ES SALAAM AONYA MACHAWA,ATAKA VIONGOZI KUFANYA KAZI KWA WELEDI

Written by mzalendoeditor

MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Dar es Salam, Khadija Ally, amesema hataki machawa na badala yake anataka viongozi na wanachama wa jumuiya hiyo kuchapa kazi.
Akizungumza leo Desemba 14, 2022 katika Ukumbi wa Karimjee, jijini Dar es Salaam Khadija amesema yeye sio mwenyekiti wa Chawa na kutaka viongozi na wanachama wa jumuiya hiyo kufanya kazi kuanzia ngazi ya Kata, kuangalia malenzi ya Watoto, maadili na elimu katika shule zinazomilikiwa na jumuiya hiyo.
“Tufanye kazi zionekane, jamii ifaidike, tuwe viongozi wenye maadili, viongozi tunapaswa kuwa mfano wa kuigwa, hatuwezi kuwa viongozi ambao hatuna maadili.” Amesema
Kufuatia hali hiyo, Khadija amesema anaandaa mafunzo maalum ya uongozi na kukumbushana misingi ya jumuiya, maadili ya uongozi na malezi.
“Sisi hatuwezi kuwa na kiongozi asiye na maadili, tuwe na uongozi shirikishi sio uongozi wa kimungu, utakachosema ndio hicho hicho hutaki ushauri, utaki kusikia lolote kwa mtu yoyote, hapana! uongozi lazima uwe shirikisho.” Amesema
Aidha, katika kikao hicho pia ulifanyika uchaguzi mdogo wa kuwania nafasi mbali mbali za uongozi ndani ya Jumuiya hiyo ambayo walioshinda nafasi ya Baraza la Mkoa na Kamati ya utekelezaji Wazazi Mkoa ni Omar Ngurangwa, Muhammad Abdulghafur na Busoro Pazi.

About the author

mzalendoeditor