Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Quincewood Group Ltd. iliyobuni mfumo wa kidigitali wa uhakiki wa pembejeo za kilimo nchini (T-Hakiki) kwa udhamini wa AGRA na MasterCard Foundation, Fatma Fernandes (kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe baada ya kufanya mazungumzo namna ya kuendelea kuboresha huduma ya upatikanaji wa lebo za kielektroniki za uhakiki wa pembejeo za wakulima nchini kwa kushirikiana na Taasisi ya Kudhibiti Ubora wa Mbegu Tanzania (TOSCI).