Featured Kitaifa

WATAFITI CHUO KIKUU HURIA CHA TANZANIA WATAKIWA KUJIELEKEZA ZAIDI KATIKA VIPAUMBELE VYA TAIFA

Written by mzalendoeditor

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Philip Mpango akitembelea mabanda ya maonesho ya tafiti zinazofanywa na Chuo Kikuu Huria cha Tanzania mara baada ya kufanya ziara ya kutembelea Chuo hicho leo Desemba 12,2022 Jijini Dar es Salaam. Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Philip Mpango akitembelea mabanda ya maonesho ya tafiti zinazofanywa na Chuo Kikuu Huria cha Tanzania mara baada ya kufanya ziara ya kutembelea Chuo hicho leo Desemba 12,2022 Jijini Dar es Salaam. Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Philip Mpango akitembelea mabanda ya maonesho ya tafiti zinazofanywa na Chuo Kikuu Huria cha Tanzania mara baada ya kufanya ziara ya kutembelea Chuo hicho leo Desemba 12,2022 Jijini Dar es Salaam.Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango akisikiliza maelezo ya matumizi ya Maabara ya Sayansi kutoka kwa  Makamu wa Mkuu wa Chuo Kikuu Huria Tanzania Profesa Elisaf Bisanda wakati alipotembelea na kukagua miundombinu ya Makao Makuu ya Chuo hicho yaliyopo Kinondoni  Jijini Dar es salaam leo tarehe 12 Desemba 2022.Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Philip Mpango (kushoto) akizungumza jambo na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda mara baada ya kufanya ziara ya kutembelea Chuo Kikuu Huria cha Tanzania leo Desemba 12,2022 Jijini Dar es Salaam. Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Philip Mpango akizungumza na wageni waalikwa pamoja na watumishi wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania mara baada ya kufanya ziara ya kutembelea Chuo hicho leo Desemba 12,2022 Jijini Dar es Salaam. Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda akizungumza mara baada ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Philip Mpango kufanya ziara chuoni Kikuu Huria cha Tanzania leo Desemba 12,2022 Jijini Dar es Salaam. Mkuu wa Chuo Kikuu Huria Cha Tanzania, Waziri Mkuu Mstaafu Mhe.Mizengo Pinda akizungumza mara baada ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Philip Mpango kufanya ziara chuoni hapo  leo Desemba 12,2022 Jijini Dar es Salaam. Mwenyekiti wa Baraza(Bodi) ya Chuo Kikuu Huria cha Tanzania Prof. Joseph Kuzilwa akizungumza mara baada ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Philip Mpango kufanya ziara chuoni hapo  leo Desemba 12,2022 Jijini Dar es Salaam.Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Huria Cha Tanzania, Prof.Elifas Bisanda akizungumza mara baada ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Philip Mpango kufanya ziara chuoni hapo  leo Desemba 12,2022 Jijini Dar es Salaam.Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (Rasilimali Fedha na Mipango) Prof.George Oreku akizungumza mara baada ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Philip Mpango kufanya ziara chuoni hapo leo Desemba 12,2022 Jijini Dar es Salaam. Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania -Taaluma, Tafiti na Ushauri wa Kitaalam Prof. Deus Ngaruko akizungumza mara baada ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Philip Mpango kufanya ziara chuoni hapo  leo Desemba 12,2022 Jijini Dar es Salaam.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango akikagua miundombinu ya Makao Makuu ya Chuo Kikuu Huria Tanzania kilichopo Kinondoni Jijini Dar es salaam leo tarehe 12 Desemba 2022.

Baadhi ya wageni waalikwa wakimsikiliza Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango baada ya kufanya ziara Makao Makuu ya Chuo Kikuu Huria Tanzania leo Desemba 12,2022 Jijini Dar es Salaam.

(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)

************************

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango ameitaka Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia hapa nchini kutoa kipaumbele cha juu zaidi katika kusaidia kukamilisha malipo ya majengo yanayotakiwa kununuliwa na Chuo Kikuu Huria Tanzania yaliopo eneo la Biafra Kinondoni Jijini Dar es salaam ili Chuo hicho kiweze kuwa na miundombinu ya kutosha.

Makamu wa Rais amesema hayo leo tarehe 12 Desemba 2022 wakati alipotembelea Makao Makuu ya Chuo Kikuu Huria Tanzania yaliopo Kinondoni Jijini Dar es salaam.

Amesema serikali itaendelea kuboresha mazingira ya chuo hicho ili kiweze kutoa elimu iliyo bora na hasa inayolenga kuwajengea wahitimu uwezo wa kujiajiri, kushindana katika soko la ajira, kuwa wabunifu na kushiriki katika fursa mbalimbali za kiuchumi.

Aidha ametoa wito kwa watafiti kujielekeza zaidi katika vipaumbele vya taifa ili kutatua changamoto mbalimbali.

Makamu wa Rais amesema ni muhimu kuendeleza jitihada za vijana walioanzisha ubunifu unaotatua changamoto ikiwemo wale wanaotumia taka katika hatua za kutengeneza chakula cha mifugo na Samaki, wanaotengeza nishati mbadala pamoja na bidhaa za lishe zinazovutia Watoto hapa nchini.

Makamu wa Rais Dkt. Mpango ameutaka uongozi wa Chuo Kikuu Huria kukabiliana na wanafunzi wanaofanya udanganyifu katika uandishi wa tafiti zao ikiwemo kutumia watu wengine katika uandishi na kupata shahada mbalimbali.

Amesema hali hiyo imeendelea kushusha hadhi ya Chuo Kikuu Huria pamoja na athari kubwa zimeendelea kuonekana katika soko la ajira ambapo wahitimu wanashindwa kukidhi mahitaji ya soko hilo.

Ameongeza kwamba ili kufikia maendeleo ya haraka ni lazima kuwekeza kwenye ubora wa rasilimali watu ambao wanatokana elimu bora.

Awali akitembelea Mabanda ya maonesho katika Chuo hicho , Makamu wa Rais ametoa wito wa kwa vyuo hapa nchini kuzalisha wahitimu watakaoweza kuendana na sekta ya ajira ikiwemo mahitaji ya sekta binafsi.

Pia ameiagiza Wizara ya Elimu , Sayansi na Teknolojia kuhakikisha vitendea kazi kwa ajili ya elimu ya Tehama kwa watu wenye mahitaji Maalum vinapatikana ili kuwasaidia kuweza kujifunza kirahisi.

Aidha ameutaka uongozi wa chuo hicho kutangaza zaidi elimu inayotolewa katika chuo hicho ikiwemo Elimu adimu ya Anga na Nyota (Astronomy).

Kwa upande wake Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof.Adolph Mkenda amesema Chuo Kikuu Huria kimeendelea kutoa fursa ya kuwafikia watanzania wengi katika maeneo walipo ili waweze kuongeza elimu yao kwa kupitia elimu ya Masafa.

Pia Prof. Mkenda amesema serikali imeendelea kutoa kipaumbele kwa elimu ya juu ikiwemo kuongeza kiwango cha mikopo kwa wanafunzi  kutoka Bilioni 464 hadi kufikia bilioni 654. Aidha ameongeza kwamba wizara hiyo itasimamia utaoaji wa haki wa mikopo kwa kuzingatia zaidi wanafunzi wenye uhitaji mkubwa.

Vilevile Prof. Mkenda amemuhakikishia Makamu wa Rais Dkt Mpango kuwa ataendelea kusimamia utoaji wa mikopo bila kutetereka ili kuwe na uwazi na utoaji wa mikopo kwa haki.

Nae Mkuu wa Chuo Kikuu Huria Cha Tanzania, Waziri Mkuu Mstaafu Mhe.Mizengo Pinda amesema walilazimika kufanya harambee ili kuweza kujenga kumbe kwaajili ya mitihani katika mikoa ya Manyara,Tabora na mikoa mingine.

Hata hivyo amemueleza Waziri wa Elimu kuwa waaangalie tafiti ambazo zimekuwa zikifanywa na Chuo hicho na kuzifanyia kazi Serikalini ili ziweze kuwa na ufumbuzi wa matatizo kutoka katika jamii yetu.

Kwa upande wake Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Huria Cha Tanzania, Prof.Elifas Bisanda ameiomba serikali kusaidia gharama za mtandao ambazo hufikia bilioni 1 kwa mwaka kutokana na utoaji wa elimu ya Masafa. Pia ametaja changamoto zinazokabili chuo hicho zikiwemo za ukosefu wa majengo katika baadhi ya mikoa hapa nchini unaohitaji shilingi bilioni 4.5 katika ujenzi wake pamoja na upungufu wa vifaa vya TEHAMA.

“Tunahitaji bilioni moja na milioni mia tisa kukamilisha ununuzi. Hili ni la dharura na haraka sana kwa sababu kuna matajiri wako tayari kulipa zaidi ya hapo, na kama si mahusiano mema kati yetu na wamiliki, eneo hilo lingeshaondoka”. Amesema Prof.Bisanda.

Prof.Bisanda amesema wanahitaji makao makuu ya chuo yenye hadhi, hivyo wameshapatiwa eneo  lenye hekari nne mkoani Dodoma huku wakikadiria kuwa kiasi cha bilioni 12 zitatosha kuweka majengo na vifaa vya msingi katika makao makuu ya chuo huko mkoani Dodoma.

Pamoja na hayo ameiomba serikali kuongeza umri wa kustaafu walimu wanataaluma wenye PhD hadi miaka 65, na miaka 70 kwa Maprofesa ambapo wengi wamestaafu wakiwa bado ni vijana, na kuendelea kufanya kazi katika vyuo binafsi huku wakiacha mapengo ambayo hayawezi kuzibwa katika vyuo  vya umma.

About the author

mzalendoeditor