Featured Kitaifa

WAZIRI MKUU KUFANYA ZIARA MKOA WA RUKWA

Written by mzalendoeditor
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Queen Sendiga akizungumza na waandishi wa habari leo mjini Sumbawanga kuhusu ujio wa Waziri Mkuu atakayewasili tarehe 14 Desemba 2022 kwa ziara ya kikazi ya siku tatu.
(Habari na Picha na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa)
……………………..

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb) atafanya ziara ya kikazi ya siku tatu (3) mkoani Rukwa kwa lengo la kukagua miradi ya maendeleo , kuongea na wananchi pamoja na watumishi wa umma.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mheshimiwa Queen Sendiga leo kwa waandishi wa habari imesema Mheshimiwa Majaliwa atawasili mkoani Rukwa tarehe 14 Desemba,2022 na atahitimisha ziara yake tarehe 16 Desemba 2022 ambapo atetembelea Wilaya tatu za Nkasi,Kalambo na Sumbawanga. 

Sendiga alibainisha  kazi zitakazofanyika kuwa ni: Kuweka jiwe la msingi ujenzi wa Shule ya Sekondari Paramawe- Nkasi,kutembelea mradi wa jengo la upasuaji na jengo la huduma za dharura (EMD) Hospitali ya Wilaya Nkasi,Kuweka jiwe la msingi jengo la Utawala Halmashauri ya Wilaya ya Kalambo, Kuweka jiwe la msingi ujenzi wa barabara ya Matai-Kasesya na Kukagua ujenzi wa Chuo cha Ualimu Sumbawanga.

Wito umetolewa kwa wananchi kujitokeza kwa wingi kwenye maeneo yatakayotembelewa na Waziri Mkuu.

Imetolewa na;

Revocatus A.Kassimba

MKUU WA KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI

About the author

mzalendoeditor