Na.Alex Sonna_MZALENDO BLOG
SIMBA wametinga hatua ya Makundi Ligi ya Mabingwa barani Afrika baada ya kuichapa bao 1_0 De Agosto ya Angola mchezo uliomalizika uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.
Shujaa wa Simba ni Moses Phiri aliyefunga bao dakika ya 33 akimalizia pasi ya HusseinTshabalala .
Kwa ushindi huo Simba wameitoa De Agosto kwa Jumla ya mabao 4_1 baada ya mechi ya awali nchini Angola kumalizika kwa Simba kushinda mabao 3-1.