Featured Kitaifa

UTEKELEZAJI WA MAAGIZO YA VIONGOZI KULETA UFANISI UTOAJI WA HUDUMA KWA WANANCHI

Written by mzalendoeditor

Asila Twaha, TAMISEMI

Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Prof. Riziki Shemdoe amesema watatekeleza maagizo yote kwa vitendo kwa lengo la kuendeleza utoaji wa huduma kwa wananchi.

Prof. Shemdoe amebainisha hayo Septemba 30, 2022 Jijini Dodoma kwenye Hafla ya Utiaji Saini Mkataba wa Usimamizi wa Shughuli za Lishe kati ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan na Wakuu wa Mikoa.

Prof. Shemdoe amemueleza Mhe. Samia kuwa ofisi yake itaendelea kushirikiana viongozi wote wa Wizara, Wadau wa Maendeleo na viongozi wa Sekretarieti za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa kwa kusimamia mkataba wa usimamiaji wa shughuli za lishe iliyosainiwa ili kuleta matokeo chanya kwa kupunguza utapiamlo nchini.

Pia Prof. Shemdoe ameongeza kuwa pamoja na kusaini mkataba huo lakini pia nikuonesha tathmin ya mkataba huo kwa kuhakikisha unatekelezwa ipasavyo na kutatua changamoto ya utapiamlo nchini.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Wakuu wa Mikoa ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mhe. John Mongela amesema wapo tayari kusimamia na kutekeleza maelekezo yote yaliyotolewa na viongozi wao kwa maslahi ya wananchi.

Aidha, Mhe. Rais kabla ya hafla ya kusaini Mkataba na Wakuu wa Mikoa alianza na zoezi la kuzindua ugawaji wa magari kwa Maafisa Elimu Sekondari, pikipiki kwa Maafisa Lishe wa Kata na Vifaa Tiba kwa ajili ya hospitali za Halmashauri ili kuleta ufanisi katika kuwahudumia watanzania.

About the author

mzalendoeditor