Featured Michezo

ARSENAL HAISHIKIKI ENGLAND YAIZAMISHA TOTTENHAM HOTSPUR

Written by mzalendoeditor
WAMEDHAMIRIA Msimu huu ndivyo unavyoweza kusema! Timu ya Arsenal imezidi kuuwasha moto katika mechi zako za  Ligi Kuu ya England baada ya ushindi wa 3-1 dhidi ya Tottenham Hotspur  Uwanja wa Emirates Jijini London.
Katika derby hiyo ya wapinzani wa Kaskazini mwa London, mabao ya Arsenal yamefungwa na Thomas Partey dakika ya 20, Gabriel Jesus  dakika ya 49 na Granit Xhaka dakika ya 67, wakati la Spurs limefungwa na Harry Kane kwa penalti dakika ya 31.
Tottenham ilimaliza pungufu baada ya Emerson kutolewa kwa kadi nyekundu dakika ya 62 kufuatia kumchezea rafu Gabriel.
Kwa matokeo hayo, Arsenal inafikisha pointi 21 na kuendelea kuongoza ligi kwa pointi nne zaidi ya Spurs baada ya wote kucheza mechi nane.
Manchester City pia ina pointi 17 na mechi moja moja mkononi katika nafasi ya pili ikiizidi Spurs wastani wa mabao.

About the author

mzalendoeditor