Featured Kitaifa

JENERALI MKUNDA:MARUFUKU MWANAJESHI KUJIHUSISHA NA SIASA.

Written by mzalendoeditor
MKUU wa Majeshi Jenerali Jacob Mkunda akifunga mafunzo ya awali ya uaskari Jeshi la ulinzi la wananchi wa Tanzania (JWTZ) Kuruti kundi la 41/22 yaliyofanyila Oljoro mkoani Arusha 
………………………………..
NA NAMNYAK KIVUYO, ARUSHA
Mkuu wa Majeshi Jenerali Jacob Mkunda amewataka wanajeshi  kutojihusisha na masuala ya siasa ikiwa ni  pamoja na kutumia mitandao ya kijamii kufanya mambo yenye manufaa badala ya kufanya mambo yasiyofaa.
Jenerali Mkunda ameyasema hayo wakati akifunga mafunzo ya awali ya askari  wa jeshi la ulinzi la wananchi  Tanzania (JWTZ ) kuruti kundi la 41/22 sherehe zilizofanyuka mkoani  Arusha ambapo alisema kuwa, huko wahitimu hao wanapokwenda watakutana na vikundi mbalimbali vinavyofanya siasa au siasa zikafanyika kwenye simu zao kupitia mitandao ya kijamii.
“Msijihusishe na siasa na hili lipo kisheria, mjue siasa ni sawa na uraibu, ukipenda siasa inakuwa ngumu sana kuacha kwahiyo nawaasa acheni kabisa kujihusisha na masuala hayo lakini pia tumieni mitandao ya kijamii kufanya mambo yenye manufaa, ninyi sijajua lakini wapo baadhi yenu waliowatangulia wanatumia mitandao ya kijamii vibaya wanatukana viongozi, wanajishulisha na siasa kama nilivyosema na Mambo mengine yasiyofaa,” Alisema Jenerali Mkunda.
“hiyo ni marufuku tukikubaini unatumia mitandao ya kijamii vibaya tutakuchukulia hatua kali lakini pia mkaishi viapo mlivyoapa kwani  mwanajeshi yoyote asiyezingatia kiapo alichoapa hatoshi kuwa mwanajeshi, mmesema mtakuwa waaminifu kwa nchi yenu, mtakuwa watifu na kuwa wanajeshi hodari kwa kufanya hivyo wataona fursa mbalimbali zikifunguka.
Alieleza kuwa wahitimu hao Wana kazi ya kulinda Katiba na uhuru wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania, ulinzi wa mipaka lakini pia kwenda kushiriki katika ulinzi wa amani ya nchi mbalimbali ambapo kwa sasa wapi DRC Congo, Lebanon na Central Africa.
Sambamba na hayo pia aliwakumbusha kuwa na nidhamu kwani ndio uti wa mgongo wa jeshi lolote Duniani na bila nidhamu hakuna jeshi ambapo aliwasihi wakienda vikosini wakikuta kuna wasio na nidhamu wasiwafuate.
Kwa upande wake mkuu wa shule Kanali Sijaona Myala alisema kuwa kati ya wahitimu hao 2457 ambao wanawake ni 606 na wanaume ni 1851, 80 wameshindwa kuhitimu mafunzo hayo kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo utoro, ugonjwa, utovu wa nidhamu, kukosa viwango na sababu zingine ambapo waliohitimu kwa kipindi chote wamelelewa katika maadili na nidhamu za kijeshi.
Aidha aliwataka kuwa na tabia njema na kuwa tayari kujirekebisha kila wanapokosea, kuwa na nidhamu na kupenda kulitumikia jeshi ikiwa ni pamoja na kujiandaa kustaafu kwa kuwa na mahusiano mazuri na wazazi,ndugu na jamii kwa ujumla na kuwa na nidhamu ya fedha.
Naye mkufunzi mkuu wa shule ya jeshi Luteni Kanali Joseph Likalangu alisema kuwa wahitimu hao 2457 wamefikia viwango vinavyokubalika na wanaenda kulitumikia taifa kwa moyo mmoja na ujasiri mkubwa kwani wamepitia mafunzo mbalimbali ikiwemo utimamu wa mwili, ukakamavu na ujasiri.
MKUU wa Majeshi Jenerali Jacob Mkunda akifunga mafunzo ya awali ya uaskari Jeshi la ulinzi la wananchi wa Tanzania (JWTZ) Kuruti kundi la 41/22 yaliyofanyila Oljoro mkoani Arusha.
BAADHI ya wanajeshi 2457 waliohitimu mafunzo ya awali ya uaskari Jeshi la ulinzi la wananchi wa Tanzania (JWTZ) kuruti kundi la 41/22 wakiwa katika gwaride.

About the author

mzalendoeditor