Featured Kitaifa

TBS YAENDESHA MAFUNZO YA AWALI UTEKELEZAJI WA MAJUKUMU YA USHIRIKIANO BAINA YA MAAFISA BIASHARA NA AFYA MKOANI DODOMA

Written by mzalendoeditor

KATIBU  Tawala wa Mkoa wa Dodoma Dk.Fatma Mganga,akizungumza wakati wa ufunguzi wa Mafunzo kwa Watumishi wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa yaliyowalenga Watumishi kutoka Idara ya Afya na Idara ya Biashara Ofisi ya Rais Tamisemi na kuhudhuriwa na  Maafisa biashara kutoka Mkoa wa Dodoma na Halmshauri zote yaliyofanyika leo Septemba 20,2022 jijini Dodoma.

……………………………….

Na Alex Sonna-DODOMA
SERIKALI imesema  inathamini suala la usalama wa chakula kwani ndio mhimili mkubwa wa afya ya watanzania na ukuaji wa uchumi.
Hayo yameelezwa leo Septemba 20 Jijini Dodoma na Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma,Dk Fatma Mganga wakati akifungua mafunzo kwa  watumishi wa Tawala za Mikoa na  Serikali za Mitaa yaliyoandaliwa na Shirika la Viwango Tanzania (TBS).
Dk Mganga amesema Serikali ya awamu ya sita inathamini suala la usalama wa chakula kwani ndio mhimili mkubwa wa Afya ya watanzania na ukuaji wa uchumi.
” Nimetonywa kwamba, kupitia mafunzo haya mtajengewa uwezo kuhusu sheria na Kanuni ya Viwango, Mwongozo wa Utekelezaji wa Majukumu ya ushirikiano baina ya TBS na Halmashauri, ukaguzi, uchukuaji sampuli na uteketezaji na utaratibu wa usombaji na usajili wa maeneo yanayotumika kuuza vyakula.
“Ni matumaini yangu kuwa mafunzo haya yataongeza umahiri wetu katika kusimamia usalama wa chakula na hivyo mtaweka mikakati madhubuti ya kusimamia maeneo yenu na kuhakikisha hakuna changamoto yoyote,”amesema Dk.Mganga.
Aidha, Sheria ya Afya ya Jamii ya mwaka 2009 na kanuni zake, sheria ya usimamizi wa usalama wa chakula na kanuni zake, pamoja na sheria ndogo za halmashauri zenu zitumike vizuri kuhakikisha maeneo yetu yanakuwa salama.
“Nichukue fursa hii kutoa pongezi nyingi kwa Serikali kukasimu baadhi ya majukumu kwa Wataalam wetu wa Halmashauri ambao wapo karibu zaidi na wadau,”amesema Katibu Tawala huyo.
Amesema kupanuliwa kwa wigo huo kutasaidia sana kufichuo vitendo viovu vilivyokuwa vinafanywa na watu wenye tamaa ya kujitajirisha kwa kuuza bidhaa ambazo hazikidhi viwango vinavyotakiwa au bidhaa zenye viambata sumu.
Amesema  sheria hiyo sasa inaenda kuwaongezea  nguvu ya usimamizi wakishirikiana na TBS na hivyo kupunguza au kuondoa changamoto zilizopo sasa.
“Niwaase mkatekeleze majukumu hayo kwa kuzingatia Sheria, Kanuni na taratibu ambazo zitafafanuliwa katika mafunzo haya.
“Sitavumilia mtaalam ambaye atafanya kinyume na kutumia mamlaka mnayokasimiwa kusumbua wazalishaji ambao wanajitahidi kuzingatia miogozo iliyopo.
“Tutumie muda wetu mwingi kuelimisha zaidi kabla ya kuchukua hatua za kuadhibu,”amesema Dk.Mganga
Aidha, amewataka kuhakikisha wakirudi  katika vituo vyao vya kazi wanatumia  mafunzo hayo vizuri.
“Hii ndio njia muafaka itakayowezesha kuhakikisha watumiaji wanapata bidhaa salama,”amesema Katibu Tawala huyo.
Kwa upande wake Meneja wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS) Kanda ya Kati,Nickonia Mwabuka amesema lengo Kuu la mafunzo hayo ni kuwapa walengwa kujua sheria,kanuni na taratibu zinazohusu utekelezaji wa majukumu baina ya Tamisemi na TBS.
Amesema mafunzo hayo yamewalenga watumishi wa idara ya afya na biashara katika Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi).
 “TBS imeekuwa ikifanya shughuli za ukaguzi na udhibiti kwa kushirikiana na watumishi kutoka katika Ofisi za Halmashauri hivyo naamini mafunzo haya yataleta ufanisi katika maeneo yao ya kazi,”amesema
Bw.Mwbuka  amesema TBS inatambua mchango wa wafanyakazi katika Ofisi mbalimbali hivyo itaendelea kutoa mafunzo kwa watumishi hao.

 

KATIBU  Tawala wa Mkoa wa Dodoma Dk.Fatma Mganga,akizungumza wakati wa ufunguzi wa Mafunzo kwa Watumishi wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa yaliyowalenga Watumishi kutoka Idara ya Afya na Idara ya Biashara Ofisi ya Rais Tamisemi na kuhudhuriwa na  Maafisa biashara kutoka Mkoa wa Dodoma na Halmshauri zote yaliyofanyika leo Septemba 20,2022 jijini Dodoma.

KATIBU  Tawala wa Mkoa wa Dodoma Dk.Fatma Mganga,akisisitiza jambo kwa washiriki (hawapo pichani)  wakati wa Mafunzo yaliyowalenga Watumishi kutoka Idara ya Afya na Idara ya Biashara Ofisi ya Rais Tamisemi na kuhudhuriwa na  Maafisa biashara kutoka Mkoa wa Dodoma na Halmshauri zote yaliyofanyika leo Septemba 20,2022 jijini Dodoma.

SEHEMU ya washiriki wakimsikiliza Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma Dk.Fatma Mganga,(hayupo pichani)  wakati wa Mafunzo yaliyowalenga Watumishi kutoka Idara ya Afya na Idara ya Biashara Ofisi ya Rais Tamisemi na kuhudhuriwa na  Maafisa biashara kutoka Mkoa wa Dodoma na Halmshauri zote yaliyofanyika leo Septemba 20,2022 jijini Dodoma.

KATIBU Tawala Msaidizi Uchumi na Uzalishaji Mkoa wa Dodoma Bi.Aziza Mumba,akizungumza wakati wa  Mafunzo kwa Watumishi wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa yaliyowalenga Watumishi kutoka Idara ya Afya na Idara ya Biashara Ofisi ya Rais Tamisemi na kuhudhuriwa na  Maafisa biashara kutoka Mkoa wa Dodoma na Halmshauri zote yaliyofanyika leo Septemba 20,2022 jijini Dodoma.

MENEJA wa Kanda ya Kati wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS) Bw.Nickonia Mwabuka,akitoa taarifa ya ufunguzi wa Mafunzo kwa Watumishi wa Tawala za Mikoa na Serikali kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa TBS Dkt.Athuman Ngenya yaliyofanyika leo Septemba 20,2022 jijini Dodoma.

Mratibu Huduma za Afya na Usafi TAMISEMI Selemani Yondu,akitoa neno la shukrani kwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma Dk.Fatma Mganga,mara baada ya kufungua Mafunzo kwa Watumishi wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa yaliyowalenga Watumishi kutoka Idara ya Afya na Idara ya Biashara Ofisi ya Rais Tamisemi na kuhudhuriwa na  Maafisa biashara kutoka Mkoa wa Dodoma na Halmshauri zote yaliyofanyika leo Septemba 20,2022 jijini Dodoma.

KATIBU Tawala wa Mkoa wa Dodoma Dk.Fatma Mganga,akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kufungua  Mafunzo kwa Watumishi wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa yaliyowalenga Watumishi kutoka Idara ya Afya na Idara ya Biashara Ofisi ya Rais Tamisemi na kuhudhuriwa na  Maafisa biashara kutoka Mkoa wa Dodoma na Halmshauri zote yaliyofanyika leo Septemba 20,2022 jijini Dodoma.

About the author

mzalendoeditor