Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhandisi Hamad Masauni amesema serikali haiwezi kuruhusu wafungwa kupata fursa ya kuonana na wapenzi wao kwa ajili ya kufanya tendo la faragha (Ndoa)gerezani kwani hiyo ni haki lakini sio haki ya msingi .
Mhandisi Masauni amebainisha hayo leo Bungeni jijini Dodoma wakati akijibu swali la mbunge aliyehoji serikali ina mpango gani wa kuruhusu wafungwa wanapata wasaa wa kufanya tendo la ndoa na wenza wao ili kuondoa upweke.
Katika majibu yake Mhandisi Masauni amesema katika tamaduni za kitanzania na Afrika kwa ujumla hazijazoea kuona mtu anapotaka kufanya tendo la ndoa na watu wengine wajue kwani hilo ni tendo la faragha.
Hivyo ,Mhadisi Masauni amebainisha kuwa kuna haki za msingi zinazoweza kuzingatiwa kwa mfungwa ikiwemo haki ya malazi,chakula na si tendo la ndoa.
“Kwa utamaduni wetu si vyema kila mtu ajue kuwa fulani anakwenda kufanya tendo la ndoa kwani tendo hilo ni la faragha hivyo,haki za msingi kwa wafungwa ni ,malazi na chakula na si haki ya tendo la ndoa akiwa gerezani”amesema.